30.7 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

Raia wanne wa kigeni waliowasili Uganda na dalili za virusi vya corona watengwa

ENTEBBE, UGANDA

RAIA wanne wa kigeni waliowasili nchini Uganda na dalili za virusi vya corona wametengwa katika hospitali ya Entebbe, Waziri wa Afya amethibitisha.

Bila ya kutaja uraia wao, ofisa uhusiano wa wizara ya afya, Emmanuel Ainebyoona alisema raia hao wamechukuliwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe.

“Sampuli ya vipimo vyao vimepelekwa katika kituo cha utafiti wa virusi nchini humo (UVRI). Na tutaitaarifu umma ” gazeti la Daily Monitor limemnukuu.

Wizara ya afya imewataka wananchi kuwa watulivu na kufuata hatua za kujikinga na ugonjwa wa corona kwa sababu hakuna udhibitisho wa kuwa virusi hivyo vimeingia nchini humo.

Aidha mwandishi wa BBC nchini Uganda amesema waziri wa afya nchini humo, ametoa agizo kwa wageni wanaotoka katika nchi zilizoathirika na virusi vya corona watengwe kwa muda wa siku 14.

Zaidi ya visa 85,000 vya ugonjwa wa virusi vya corona vimethibitishwa katika nchi 57 kote duniani huku vifo 3,000 vikithibitishwa, kulingana na Shirika la Afya Duniani.

Idadi kubwa ya vifo hivyo vimetokea China ambako virusi hivyo vilianzia mwishoni mwaka jana.

Marekani  ni miongoni mwa nchi zilizothibitisha kifo baada ya juzi mtu mmoja kufariki dunia kwa virusi hivyo katika jimbo la Washington.

Maofisa wamesema mgonjwa huyo aliyekuwa na miaka 50, alikuwa mwanaume ambaye hali yake ya afya haikuwa nzuri.

Rais Donald Trump  wa Marekani amesema kwamba visa vingi zaidi vinatarajiwa kutokea na akaongeza kuwa nchi hiyo imejitayarisha kwa lolote litakalo tokea.

Jumapili, Australia na Thailand pia zilirekodi kifo cha kwanza cha virusi vya corona.

Mwanamume wa miaka 78 wa Australia aliaga dunia baada ya kuambukizwa ugonjwa huo katika meli ya Diamond Princess nchini Japan mwezi uliopita.

Thailand ambayo imethibitisha visa 42 vya virusi vya corona inasema mwanaume wa miaka 35, aliyekufa pia  na alikuwa anaugua homa ya dengue.

UWEZEKANO WA MTU MWENYE VIRUSI KUFA

Utafiti wa sasa unakadiria kuwa kati ya kila watu 40, watu watano wana virusi vya corona na watu 1,000 wanaweza kufa kutokana na ugonjwa huo, au asilimia moja ya watu 1000.

Siku ya jumapili, waziri wa afya Matt Hancock alisema Serikali ya Uingereza itafanya uchunguzi vizuri na kuangalia idadi hiyo ya vifo kuwa chini ya asilimia mbili au chini ya hapo.

Ingawa huwa inategemea na sababu kadhaa kama umri, jinsia na hali ya afya ya mtu pamoja na mfumo wa afya uliopo sehemu husika.

Katika kiwango cha elimu ya juu ni ngumu kubaini idadi ya watu wanaopoteza maisha kutokana na virusi vya corona.

Hata kuhesabu visa vya ugonjwa huo ni ngumu pia.

Kesi nyingi za ugonjwa huo huwa hazifahamiki kwa sababu watu wana tabia ya kutokwenda kwa daktari wanapopata dalili za ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na chuo cha Imperial, mataifa mbalimbali yako kwenye nafasi nzuri au mbaya ya kubaini maambukizi hayo kwa kuwa ni ngumu kuhesabu visa vya ugonjwa huo.

UKO KWENYE HATARI GANI YA KUAMBUKIZWA?

Baadhi ya watu wako kwenye hatari ya kufa wakipata maambukizi ya virusi vya corona tofauti na wengine.

Watu hao ni wazee, wagonjwa na wanaume pia.

Katika utafiti wa kwanza uliojumuisha kesi 44,000 nchini China, idadi ya vifo ilikuwa kubwa mara kumi zaidi kwa wazee kuliko watu wenye umri wa kati.

Idadi ya vifo iko chini kwa watu wenye umri wa chini ya miaka 30-kulikuwa na vifo nane katika kesi za wagonjwa 4,500.

Na vifo hivyo viliwatokea mara tano zaidi atu ambao wana ugonjwa wa kisukari , ugonjwa wa moyo au wenye matatizo ya kupumua.

Kuna idadi kubwa ya vifo vya wanaume ukilinganisha na wanawake.

Sababu zote hizo ukizijumisha watalaamu wanasema bado hawawezi kupata picha kamili ya mtu ambaye yuko kwenye hatari katika kila eneo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles