27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Hospitali yakaribia kutibu saratani

Asha Bani -Dar es Salaam

MKURUGENZI wa Hospitali ya Narayana Health kutoka nchini India, Dk. Sunil Bhat ameielezea hospitali hiyo uwezo wa kutibu ugonjwa wa saratani, baada ya kuleta matumaini ya afya kwa mtoto Ittai James (4), aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo muda mrefu.

Ittai aliyekuwa akiugua saratani ya tumbo, ameonyesha dalili za kupona baada ya madaktari bingwa wa hospitali hiyo kuthibitisha afya yake, baada ya kumfanyia upandikizaji wa uloto.

Baba wa mtoto huyo, James Moshi pamoja na madaktari wake, akiwemo mkurugenzi wa Hospitali ya Narayana, walisema Ittai alipandikizwa uloto Septemba, mwaka jana nchini India na ndipo alianza kuonyesha dalili za kupona.

Alisema Ittai, alikuwa kwenye hatua ya mwisho ya ugonjwa huo, lakini hospitali imefanikiwa kumpa tiba iliyoonyesha mafanikio kwake na kurudisha faraja kwa wazazi pia.

Akizungumza na gazeti hili, baba wa Ittai, alisema amezunguka hospitali mbalimbali na mwanae, lakini hakuna matibabu ambayo yalimsaidia na ndipo alielekezwa kwenda India.

Alisema mtoto wake alianza na dalili za kusumbuliwa na homa kali, mwili na maumivu ya tumbo mara kwa mara kiasi cha kukosa raha katika maisha yake.

Kuhusu upasuaji wa mtoto kabla ya kumpandikiza uloto, Dk. Bhat alisema walimwondoa uvimbe uliokuwa na dalili za saratani Julai, mwaka jana  na Septemba wakampandikiza seli za damu kutoka kwenye uloto wa mwilini mwake.

Pia alizungumzia huduma hiyo kwamba wanaokwenda kutibiwa nje, ni Sh milioni 200 kwa anayepandikizwa uloto kutoka kwa ndugu yake, wakati kwa anayepandikiza kutoka kwake mwenyewe ni Sh milioni 150.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,554FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles