29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga wanyoosha mikoni ubingwa VPL

Zainab Iddy, Dar es Salaam

UONGOZI w Yanga, umesema kuwa kwa sasa akili zao wanazielekeza katika ubingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho la Tanzania (ASFC) kwani nafasi yao ya kubeba ‘mwali’ wa Ligi Kuu Tanzania Bara ni ndogo.

Kauli hiyo ya Yanga imekuja baada ya juzi kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya ASFC kwa kushinda bao 1-0 dhidi ya Gwambina kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Yanga imeungana na Simba, Azam, Alliance, Namungo, Ndanda, Sahare na Kagera Sugar katika hatua ya robo fainali, zikiwa zinasubiri droo iliyopangwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema japo bado hawajakata tamaa ya mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara, lakini kutokana na asilimia ndogo waliyonayo katika hilo, wameona heri kuelekeza nguvu zaidi ASFC.

“Kulingana na michezo tuliyocheza na tofauti yetu ya pointi na timu inayoongoza ligi, hatuwezi kujipa matumaini makubwa kuwa tutachukua ubingwa msimu huu, lakini huku katika FA (ASFC), iwe jua au mvua, utakuja kwetu.

“Hatuwezi kuliacha kombe hili kirahisi wakati nafasi ya kulichukua tunayo, tunajua kila timu inalitolea macho, lakini kwa sababuYanga wote tumeamua kupita njia moja, hakuna kitakachotushinda, fainali tutaingia na taji tutalichukua,” alisena Mwakalebela.

Mwakalebela aliongeza kuwa wanatambua timu zote zilizoingia hatua ya robo fainali si za kuzibeza, lakini kutokana na mipango mikakati wanayoanza kuijenga sasa, hakuna kitakachowashinda.

Katika msimu uliopita, Yanga ilitolewa hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo na Lipuli FC ya Iringa baada ya kufungwa mabao 2-0 mechi iliyochezwa Uwanja wa Samora, Iringa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles