25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Wagombea ACT kujulikana Machi

BRIGHITER MASAKI-DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha ACT- Wazalendo, Omar Said Shaaban, amesema hatua inayofuata baada ya mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu kukamilika ni mchujo wa wagombea utakaofanyika kati ya Machi 1 na 2.

Akitoa taarifa ya mwenendo wa uchukuaji na urejeshaji fomu za kuwania nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho jijini Dar es salaam jana, Shaaban alisema mchakato huo ulikamilika Februari 26 baada ya kudumu kwa mwezi mmoja.

“Zaidi ya wanachama 200 kutoka maeneo mbalimbali wamechukua na kurejesha fomu za kuomba uongozi ngazi mbalimbali. Kwa utaratibu wa kanuni za uchaguzi za chama majina haya yatapelekwa kwenye vikao vya uteuzi.

“Kikao cha kwanza kitakuwa ni Kamati Kuu kitakachoketi  Machi Mosi na kuteua majina ya wagombea wa nafasi zote  za ngome. Kutakuwa na kikao cha halmashauri kuu kitakachofanyika Machi 2 ambacho kitatuea majina ya wagombea waliomba nafasi ya za kitaifa ndani ya chama, “alisema Shaaban.

Alisema baada ya majina ya wagombea hao kupitisha katika ngazi hizo, kitakachofuata ni kampeni za watia nia zitakazodumu kwa siku saba.

Uchaguzi wa viongozi wakuu utafanyika Machi 14, ukitanguliwa na chaguzi nyingine za ngome ya wazee, utakaofanyika Machi 7 na Machi 8 ngome ya wanawake.

Nafasi zinazogombewa katika uchaguzi huo ngazi ya taifa ni pamoja ni kiongozi wa chama, naibu kiongozi, mwenyekiti wa taifa, makamu mwenyekiti Bara na Zanzibar, katibu mkuu, wajumbe wa halmashauri kuu (nafasi 15) na wajumbe wa kamati kuu (nafasi nane).

Ngome ya wanawake nafasi zinazogombewa ni mwenyekiti wa ngome, makamu mwenyekiti wa ngome, katibu na wajumbe wa halmashauri kuu (nafasi 15) na wajumbe wa kamati kuu (nafasi nane).

Wakati ngome ya vijana nafasi zinazogombewa ni mwenyekiti, makamu mwenyekiti Bara na Zanzibar, katibu na naibu wake, wajumbe wa halmashauri kuu taifa na wajumbe wa mkutano mkuu.

Miongoni mwa waliochukua fomu kugombea nafasi ni pamoja na Maalim Seif Sharif Hamad na Yeremia Maganja  (uenyekiti), Zitto Kabwe na Ismail Jussa  (kiongozi wa chama), Juma Duni Haji (makamu mwenyekiti  Zanzibar), Dorothy Semu  na Riziki  Ngwali (makamu mwenyekiti bara).

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles