29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mahiga: Serikali itenge bajeti kamati za maadili

Mwandishi Wetu -Dodoma

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk. Augustine Mahiga ameiomba Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kutenga bajeti kwa kamati za maadili za maofisa wa mahakama za mikoa na wilaya ili ziweze kutekeleza majukumu yake kama sheria inavyozitaka.

Kamati za maadili za maofisa wa mahakama zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya kutotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria kutokana na upungufu wa bajeti. 

Kamati hizo ziliundwa baada ya kutungwa Sheria ya Usimamizi wa Mahakama namba 4 ya mwaka 2011.

Akizindua mwongozo wa uendeshaji wa kamati hizo Dodoma juzi, Dk. Mahiga alisema Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria itahakikisha Tume ya Utumishi wa Mahakama inapatiwa rasilimali fedha kuendesha shughuli zake, ikiwamo kamati za maadili za maofisa wa mahakama kwa ufanisi unaotakiwa.

Aliwataka wajumbe wa kamati hizo kuutumia mwongozo wa uendeshaji kuondoa changamoto mbalimbali zilizokuwapo, kwani matarajio ya tume na Serikali ni kuona utekelezaji wa majukumu unaozingatia matakwa ya sheria, kanuni na taratibu.

Alisema kwa kuona umuhimu wa kuimarisha dhana ya utawala bora kupitia sheria ya uendeshaji wa mahakama, Serikali imeruhusu uwepo wa kamati hizo ambazo ni pamoja na kamati ya maadili ya majaji, kamati ya maadili ya maofisa wa mahakama na kamati ya maadili ya mahakama ya mkoa na wilaya.

Dk. Mahiga alisema kamati hizo zina nafasi kubwa kusimamia, kuendeleza na kudumisha maadili ya utumishi wa mahakama.

Alisema suala la kuwapatia wajumbe wa kamati mwongozo huo, ni la msingi kwani sasa watatekeleza majukumu yao kwa kufuata msingi wa sheria, kanuni na taratibu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles