26.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Wataalamu kujadili maendeleo ya kilimo

Ramadhan Hassan -Dodoma

WATAALAMU wa kilimo, watafiti na wajasiriamali, wanatarajia kujifungia kwa siku mbili jijini hapa kujadiliana jinsi ya kukiendeleza kilimo cha Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi jijini hapa, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wachambuzi na Watafiti wa Sera za Kilimo, Audax Rukonge alisema watakuwa na kongamamo hilo litahusu utekelezaji wa masuala mbalimbali kwenye sekta ya kilimo.

Alisema kongamano hilo litakuwa ni la sita ambapo watajadiliana kuhusu ukuaji wa sekta ya kilimo, jitihada za mabadiliko ya kisera, haja ya kuweka vipaumbele katika sekta ya kilimo, pamoja na kutumika kwa vipaumbele.

Aliyataja mambo mengine watakayojadiliana ni pamoja na sera ya sekta ya kilimo, biashara na uwekezaji katika kilimo, uzalishaji kwenye sekta binafsi hasa kwenye tija, upatikanaji wa pembejeo na matumizi ya teknolojia.

“Pia tutajadiliana upatikanaji wa fedha na huduma saidizi mfano katika ugani na nishati, tutajadiliana katika suala zima la ardhi, mazingira na maliasili na katika mazingira na masuala ya tabia nchi na la mwisho ambalo ni kubwa tutaangalia suala la usalama wa chakula,” alisema Rukonge.

Alisema ukuaji wa sekta ya kilimo bado umeendelea kukabiliwa na changamoto ya tija ambayo imekuwa ipo chini, hivyo katika kongamano hilo watajadiliana kwa kina wanatakiwa kufanya nini.

“Kuna changamoto ya uongezwaji wa thamani katika mazao bado ni mdogo ndiyo maana Serikali ya awamu ya tano imekuja na kaulimbiu ya uanzishwaji wa viwanda ili thamani ya mazao iweze kuonekana,” alisema Rukonge.

Mchambuzi wa sera za kilimo, Aisack Minde, alisema mafaniko ya makongamano matano yaliyopita ni pamoja na kuweza kuongeza uhusiano mzuri kati ya sekta binafsi na ya umma.

“Tumeweza kuongeza uhusianpo mzuri kati ya sekta ya umma na binafsi mwaka  2014 ukilinganisha na mwaka 2020 mahusiano hayakuwa kama leo, tumechangaia kwa kiasi kikubwa kwenye jambo hili,” alisema Minde.

Alisema katika tozo ya mazao kulikuwa na changamoto ya tozo kuwa nyingi na wao walipaza sauti na Bunge kupunguza kutoka tano hadi tatu.

“Watu wakati mwingine hawafamihani, lakini tumefahamiana, kupitia makundi hayo watafiti na wanataaluma wamekutana na kujadiliana kwa pamoja, haya ni mafanikio makubwa kwetu,” alisema Minde.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,628FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles