29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Chama cha Walimu chapata msaada wa bilioni 1/-

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

SHIRIKAl la kimataifa lisilo la kiserikali la Helvetas limetoa Sh bilioni 1.15 na Chama cha walimu Tanzania (CWT) kimetoa Sh milioni 300, kwajili ya kuchangia kutimiza lengo la kusaidia walimu kitaaluma linatimia na kuwa endelevu kupitia mradi wa SITT.

Mradi huo wa SITT 2019-2021, unalenga katika kuboresha mbinu za kufundishia hasa kwa walimu wa shule za msingi ulizinduliwa jana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk. Avemaria Semakafu jijini Dodoma.

Akizungumza jkatika uzinduzi huo, Meneja wa mradai huo, Donatian Marusu, alisema kuwa kiasai hicho cha fedha ni sehemu ya kutimiza jukumu la kuhakikisha kuwa lengo la kusaidia walimu kitaaluma na kuwa endelevu.

Alisema kupitia mradi huo zaidi ya walimu 285, na walimu wakuu 95, kutoka  mikoa ya kati na walimu 130 na walimu wakuu 130, kutoka mikoa ya kaskazini watanufaika na mradi huo.

Pia alisema zaidi ya wanafunzi 49,000 katika mikoa ya kati na wanafunzi 61,000 kutoka mikoa ya kasakazini watanufaika na mafunzo ikiwa ni pamoja na kupatiwa vitabu vya hisabati na sayansi ya mazingira.

“Mgeni rasmi tunayofuraha kubwa kukukaribisha lkatika mkutano huu wa wadau wa elimu kwajili ya kuutambulisha mradi wa Inclussive School-based In-services Teacher Traing mbao kwa kifupi hujulikana Iclusive SITT, ambao utatekelezwa katika mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora na Shinyanga,” alisema

Aidha alisema kuwa mradi huo umekuja kutokana na ombi la wadau kutaka kupanua kutoka mikoa ya kasakazini yaaani Arusha, Manyara na Kilimanjaro na kuoengeza mingine mnne.

Vilevile, alisema kuwa wakufunzi wa hisabati 24, kutoka vyuo hivyo watapatiwa mafunzo ya mbinu na ufundishaji somo hilo na watakabidhiwa jukumu la kwenda kutoa mafunzo kwa walimu na walimu wa shule za msingi zinazozunguka vyuo vyao.

Kwa upande wake Naibu katibu mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk. Avemaria Semakafu aliwataka walimu waliopata nafasi ya kuwa sehemu ya mradi huo kuwa chachu ya mafanikio katika maeneo yao kwa kuboresha ufundishaji.

“Tatizo kubwa tulilonalo ni changamoto ya mbinu za kufundishia  programu hii ikasaidie katika kuboresha namna bora ya ufundishaji katika shule zetu ili kuboresha utoaji wa elimu nchini”alisema Dk. Semakafu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles