24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

Miradi ya JUMEME yaziondoa gizani kaya 5,000 Ukerewe

MWANDISHI WETU

ZAIDI ya kaya 5,000 katika kisiwa cha Ukara kilichopo wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, zimenufaika na umeme jua unaozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya usambazaji umeme vijijini (JUMEME).

Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo, Profesa Costa Mahalu katika hotuba yake kwa maofisa kutoka Umoja wa Ulaya na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), waliotembelea miradi ya umeme jua iliyopo wilaya hapo.

Profesa Mahalu alisema kaya hizo zimenufaika kutokana na awamu ya kwanza ya mradi wa usambazaji umeme katika kisiwa hicho cha Ukara.

Baadhi ya mafundi mitambo wa kampuni ya JUMEME, wakifunga mitambo ya umeme jua katika moja ya miradi ya kampuni hiyo huko kisiwani Ukara, Ukerewe mkoani Mwanza.

“Awamu ya kwanza ya iliyopewa jina la “Uzalishaji umeme wa katika kukuza uchumi wa Tanzania’ imeonesha utofauti kutokana na faida za kiuchumi na kijamii zilizopatikana.

“Kwa sababu mbali na kaya 5,000 kunufaika pia, wafanyabiashara wadogo na viwandani pia wameunganishwa. Lakini taasisi mbalimbali zinazotoa huduma za kijamii kama vile maji vijijini na hospitali zimeunganishwa,” alisema.

Alisema huduma za JUMEME zimevifikia vijiji 20 kwenye visiwa 10 tofauti, na kuchochea uchumi wa eneo hilo jambo lililosaidia kuibua fursa nyingi za ajira.

“Malengo ya muda mrefu kwa JUMEME ni kuendelea  kushirikiana na wazalishaji wadogo ikiwa ni pamoja na kuwekeza kwa waajiriwa wa eneo husika,” alisema Prof. Mahalu ambaye pia ni Makamu wa Chuo Kikuu cha Mt. Agustino (SAUT).

Aidha, alisema kampuni hiyo imekuwa ikizingatia utoaji wa fursa za ajira kwa watanzania ili kuisaidia Serikali kukabiliana na uhaba wa ajira kwa vijana nchini.

“Kila mmoja wa wafanyakazi wanaofanya kazi ya uhandisi katika miradi 12 ya JUMEME, ni Mtanzania. Kati ya watu 25 wanaounda timu ya kudumu ya JUMEME wenyeji ni 22, ambao hupewa upendeleo wa wazi linapokuja suala la kufanya kazi.

“Kwa kuzingatia mafanikio ya awamu hii ya kwanza, tunatumaini kuwa na uwezo wa kutoa fursa zaidi za kazi kwa vijana wetu kwa kuendelea nao katika awamu ya pili, ya tatu na kuendelea zaidi katika miradi ya JUMEME. ” alisema.

Alisema ili kuongeza uweledi na ufanisi wa waajiriwa wazalendo, kampuni hiyo inaendelea kutoa mafunzo yanayowajengea uwezo wahandisi wa ndani na vijana wataalamu kwa madhumuni ya kuendesha gridi ndogo ndogo zinazoendelea kujengwa hapa nchini.

Pia alisema lengo la JUMEME ni kutoa umeme wa uhakika na wa bei nafuu kwa wakazi husika hususani maeneo ambayo umeme gridi ya Taifa haiwezi kufika.

“Lengo letu ni kufunga mifumo 300 ya uzalisha umeme utakaoweza kuingizwa kwenye ya gridi ya Taifa na kusaidia watu zaidi ya 1,000,000 ifikapo mwaka 2023 katika vijiji mbalimbali nchini Tanzania.

Aliongeza kampuni hiyo ya JUMEME ilioundwa mwaka 2014  chini ya mradi wa “Micropower Economy roll out in Tanzania” na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU), inalenga kukuza, kujenga, na kuendesha gridi ndogo za umeme jua katika vijijini mbalimbali  nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles