TWALAD SALUM-MWANZA
WAKAZI wa Kijiji cha Nyashishi kata ya Usagara wilayani Misungwi Mkoani Mwanza, wamehukumiwa kwenda jela kila mmoja miezi 18 baada ya kukili tuhuma ya wizi.
Kutokana na hali hiyo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Misungwi, Esther Maliki amewahukumu Yohana Charles (21) ambaye alikiri kuvunja na kuiba na Said Ally (20) ambaye alikamatwa na mali inayodaiwa kuwa ya wizi .
Washatakiwa wote wawili walikuwa wakikabiliwa na kesi ya jinai namba 91 ya mwaka 2019 ambapo walihukumiwa kutumikia kifungo cha miezi 18 kwa kila mmoja baada ya kukili kosa la kuvunja na kuiba vitu vya thamani ya Sh milioni 4 .2
Mahakama iliwatia hatiani baada kila mmoja kuwa amekili kutenda kosa, na kuangalia kumbukumbu za nyuma za makosa kulikuwa hakuna, mshitakiwa wa kwanza Yohana Charles aliyekili kuvunja na kuiba mali ya Omari Kibwinya mkazi wa Kijiji cha Nyashishi.