25.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Waenda jela kwa kukili kuhusika na wizi

TWALAD SALUM-MWANZA

WAKAZI  wa Kijiji cha Nyashishi kata ya Usagara wilayani Misungwi Mkoani Mwanza, wamehukumiwa kwenda jela kila mmoja miezi 18 baada ya kukili tuhuma ya wizi.

Kutokana na hali hiyo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Misungwi, Esther Maliki amewahukumu Yohana  Charles (21) ambaye alikiri kuvunja na kuiba na Said  Ally (20)  ambaye alikamatwa na mali inayodaiwa kuwa ya wizi .

Washatakiwa wote wawili walikuwa wakikabiliwa na kesi ya jinai namba 91 ya mwaka 2019 ambapo walihukumiwa kutumikia kifungo cha miezi 18  kwa kila mmoja baada ya kukili kosa  la kuvunja na kuiba vitu vya thamani ya Sh milioni 4 .2

Mahakama iliwatia hatiani baada kila mmoja kuwa  amekili kutenda kosa, na kuangalia kumbukumbu za nyuma za makosa kulikuwa hakuna, mshitakiwa wa kwanza  Yohana Charles aliyekili kuvunja na kuiba mali ya Omari Kibwinya mkazi wa Kijiji cha Nyashishi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,526FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles