FERDNANDA MBAMILA, DAR ES SALAAM
Kampuni ya Coca cola nchini kupitia mmoja wa washiriki wake Coca cola kwanza imekabidhi zawadi kwa wanafunzi katika Mkoa wa Dar es Salaam baada ya shule hizo kukusanya chupa za plastiki kupitia kampeni ya Copa Coca cola ya rejesha na ushinde.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Coca cola kwanza, Josephine Msaliwa aliwasihi na kuwahamasisha wanafunzi na watanzania kwa ujumla kuendelea kushiriki kampeni za ukusanyaji wa chupa za plastiki na kampeni nyingine za namna hiyo ili kupunguza taka na kujenga mazingira safi na yenye afya.
Alisema kwa shule zilizoshinda katika uokotaji wa makopo ya plastiki zilikusanya zaidi ya chupa kilo 880,835 kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Iringa ambapo shule ya sekondari Kihesa ilipata idadi kubwa zaidi ya ukusanyaji wa chupa za plastiki na kushinda zawadi kubwa ambayo ni urekebishaji wa kiwanja cha mpira na zawadi nyingine mbalimbali.
Sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu mashindano ya Coca cola yalikuwa zaidi ya mpira wa miguu kwa shule zote zilizoshiriki.
Aidha mashindano yalijikita zaidi katika kubadili tabia kwa wanafunzi kwa kuja na kampeni ya ukusanyaji kama sehenu ya kuwaelimisha juu ya umuhimu wa usafi wa mazingira kupitia ujusanyaji wa chupa.
Kwa Mkoa wa Dar es Salaam shule tatu zilifanya vizuri ikiwa ni pamoja na shule ya Sekondari ya Kisarawe 11 ya Wilaya ya Kigamboni , Shule ya Sekondari ya Kambangwa ya Kinondoni na shule ya Sekondari ya Mikwambe ya Wilaya ya Temeke.
“Wanafunzi wa shule hizo tajwa walikusanya kiasi cha chupa za plastiki kilo 7,052, 6,279 na 3, 110 hiyo ni wakati wa kampeni na ambapo siku ambapoyo walipewa zawadi ya jezi 32 za COPA Coca cola na mipira 2 kwa kila shule.
Pia wanafunzi watatu kutoka kila moja ya shule zilizoshinda, walipewa zawadi za Tablet na saa kwa kuwa na ushawishi mkubwa katika shule zao, huku waalimu watatu kutoka kula shule wakiondoka na zawadi za Laptop, beg na fulana za Coca cola.
Alisema ukusanyaji wa chupa haulindi tu maliasili ya ulimwengu lakini pia husaidia kuleta maisha bora kwa kila mtu.
“Kama kampunu ya Coca cola tuliona ni sawa kuhamasisha wanafunzi wanaoshiriki katika COPA Coca cola kushiriki katika ukusanyaji wa chupa za plastiki kutoka kwenye umri mdogo ili kuleta mabadiliko ya tabia ndani yao katika maisha yao yote,” alisema Josephine.