28.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Daktari wanawake afikishwa mahakamani kwa kuwaondoa viungo wakati wa upasuaji

VIRGINIA, MAREKANI

DAKTARI bingwa wa kina mama, Javaid Perwaiz anatuhumiwa kwa kufanya upasuaji kwa wanawake na kutoa viungo bila ridhaa zao.

Mmoja wa wagonjwa wake amemtuhumu na kumfikisha mahakamani huko Virginia nchini Marekani.

Dk. Perwaiz anadaiwa kuwadanganya  wanawake kuhusu afya zao na kuwasababishia majeraha makubwa, kwa mujibu wa Shirika la Upepelezi la Marekani (FBI).

Tangu kukamatwa kwake Novemba 8 mwaka huu, zaidi ya wanawake 126 wameripoti na kulalamika kuhusu tabia zake.

Alhamisi wiki hii Jaji wa mahakama alitoa amri ya kukamatwa kwa Dk. Perwaiz wakati akisibiri hukumu yake.

Kwa mujibu wa hati ya kukamatwa ya FBI Dk.Perwaiz anatuhumiwa kutoa majibu ya uongo ya kiafya na kufanya upasuaji usio wa lazima kwa wagonjwa wake na bila ridhaa zao.

Amefanya upasuaji wa kutoa sehemu za uzazi za wanawake bila ridhaa zao pamoja na kufunga uzazi. 

Daktari huyo ana ofisi mbili eneo la Chesapeake, jimbo la Virginia nchini Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa zilizofikishwa mahakamani, katika kipindi cha mwaka 2014- 2018 Dk. Perwaiz amefanya upasuaji kwa asilimia 40 ya wanawake wanaopokea matibabu wakiwa na kipato cha chini.

Inadaia kuwa katika kundi la wagonjwa wanawake 510, asilimia 42 walifanyiwa angalau upasuaji wa aina mbili.

Shirika la upepelezi la FBI lilipewa taarifa kwa mara ya kwanza mwaka 2018 na muuguzi ambae alisikia kutoka kwa mgonjwa mmoja.

”Wagonjwa wanasema kuwa walikua wakisikia Dk. Perwaiz akitaja sana kuhusu saratani na kuwatisha waweze kufanyiwa upasuaji” anasema Ofisa wa FBI, Desiree Maxwell.

Wakili wa Dk. Perwaiz hakujibu baada ya kutafutwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza wiki hii baada ya kupata taarifa hizo.

Inaelezwa kuwa Dk Perwaiz amesoma masomo yake ya utabibu huko Pakistani na alipata leseni ya kufanya kazi Virginia Marekani mwaka 1980.

Mwaka 1982 alipoteza sifa zake za kufanya kazi katika hospitali huko Maryland kutokana na maamuzi mabaya ya kitabibu.

Kwa mujibu wa FBI alifanyiwa uchunguzi mara ya kwanza na bodi ya madaktari wa Virginia kwa kufanya upasuaji bila kuwa na maamuzi yasiyo na weledi wa kitaaluma.

Baada ya kukubali hatia ya kukwepa kodi 1996, alinyang’anywa leseni kwa miaka miwili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,908FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles