27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wanawake wanaokwenda vilabuni na watoto hatarini

FRANCIS GODWIN-IRINGA

JUKWAA la Utetezi na Ujasiriamali la Wanawake wa Kijiji  cha Kilalakidewa wilayani Kilolo mkoani Iringa kwa  kushirikiana na uongozi wa Serikali ya kijiji  hicho wameweka utaratibu wa kuwawajibisha wanawake wanaonyanyasa  waume zao na wanaokwenda na watoto  wadogo kwenye vilabu vya pombe na kisha kuwanywesha.

Akizungumza  wakati wa tathimini ya mradi wa haki sawa ya  umiliki wa mali mbalimbali na ardhi kwa wanawake  iliyofanywa na asasi isiyo ya kiserikali ya Iringa Civil Society Organizations (ICISO) jana na Katibu wa Jukwaa hilo, , Stumai Kapenea ambapo alisema kuwa wamelazimika kuungana na kijiji kuweka sheria ya kukomesha unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto na wanaume wanaonyanyasika na wake zao.

Kuwa wapo wanaume ambao wamekuwa wakinyanyasika na wake zao kwa kunyimwa haki yao ya ndoa pia kudhalilishwa kwa matesi baada ya wanawake hao kulewa pombe .

Hivyo kutokana na vitendo hivyo kushamiri na baada ya kupewa elimu na asasi ya ICISO  kupitia mradi wake wa haki sawa ya usimamizi wa mali mbali mbali ,ndipo wanawake wa kijiji hicho walipoamua kuanzisha jukwaa lako kwa msaada wa shirika hilo .

“Mwanzoni kabla ya jukwaa kuanza wanaume walikuwa wakivumilia mateso na kasi ya watoto kwenda kunyweshwa pombe vilabuni ilikuwa kubwa ila sasa hakuna mtoto anayeonekana kilabuni na wanaume wanaishi kwa amani bila manyanyaso,” alisema

Alisema suala la unyanyasaji lipo pande zote mbili wapo wanawake wanaonyanyasika na wanaume zao nao wamekuwa wakibanwa sawa na wanawake wanaonyanyasa waume zao .

Aidha alisema jukwaa hilo pia limeanzisha mradi wa kiuchumi wa ufugaji wa kuku za kienyeji na kilimo cha mazao ya biashara ili kujikwamua kiuchumi .

Kwani alisema kupitia miradi hiyo wana uhakika wa kuboresha maisha yao kwa kusaidiana kiuchumi na pia kuwasaidia watoto wanaohitaji msaada hasa wale yatima .

Hata hivyo alipongeza ICISO kwa kutoa elimu ya haki sawa kupitia mradi wa haki sawa ya umiliki wa mali kwa wanawake na watoto ambapo kupitia elimu hiyo wananchi unyanyasaji unaotokana na mali umepungua.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Michael Chambili, alisema kuwa jukwaa hilo limekuwa likitoa msaada mkubwa kwa serikali ya kijiji hicho kwani wao jukumu lao ni kupokea malalamiko na kuwasikiliza na pale inaposhindikana wanapeleka ofisi ya kijiji ambako wanahusika hupewa adhabu iliyopendekezwa na serikali ya kijiji.

Alisema kupitia ushirikiano huo kijiji kimekuwa kikiishi kwa utulivu kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake na kuwa wale ambao wamekuwa wakipatikana na hatia na kushindwa kulipa faini wameishia kukimbia kijiji.

Mtendaji Mkuu wa ICISO, Raphael Mtitu alisema lengo la mradi huo ilikuwa ni kuwajengea uwezo wanawake katika kutambua wajibu wao wa kumiliki mali mbali mbali pia jamii nzima kuwa na utamaduni wa kuandika wosia kabla ya kifo ili kuepusha migogoro ya kugombea mali baada ya kifo .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles