32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mnyeti aagiza wachimbaji madini Kiteto wakamatwe

Mohamed Hamad

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ameagiza Jeshi la Polisi wilayani Kiteto kuwakamata wanachimbaji wa madini aina ya rubi, Kijiji cha Orgine kwa kufanya shughuli hiyo kinyume cha sheria.

Mnyeti ametoa agizo hilo baada ya lalamikiwa na wananchi hao kuwa hawanufaiki na shughuli ya uchimbaji wa madini Kijijini hapo huku wachimbaji wakiendelea kuneemeka.

Akiwasilisha kero hiyo, Jafari Yasini amesema, kijiji cha Orkine hakinufaiki na uchimbaji, hata vifusi vya kufukia msingi katika miradi ya ujenzi wanalazimika kununua kutoka kwa wachimbaji hao.

Mkuu wilaya ya Kiteto Tumaini Magessa, alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema kuwa, wilaya ilishawaandikia barua wachimbaji na kushangazwa kusikia lalamiko hilo kuwa kazi hiyo inaendelea.

“Tuliwaandikia barua hawa wachimbaji wa madini aina ya rubi hapa Kijiji cha Orkine baada ya kubaini kuanza kunufaika na madini haya ingawa hawataki kuonyesha nufaiko hilo wakidai bado wako kwenye majaribio kipindi chote”alisema Magessa.

Akitoa agizo hilo Mnyeti alimwagiza Mkuu wa Polisi Kiteto, Fadhili Luoga kuwakamata wachimbaji hao mara moja na kuandaliwa mashitaka ili waweze kujibu tuhuma kwanini waendeleze uchimbaji kinyume cha sheria.

“OCD ninakuagiza nenda ukawakamate hawa wachimbaji wa madini haya, haiwezekani waendelee kuchimba kwa zaidi ya miaka 20 bila kulipa kodi hali hii halikubaliki hata kidogo”me sema Mnyeti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles