23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Vijana waaswa kufanya kazi kwa bidii

Upendo Mosha, Moshi

Katibu wa Baraza Kuu la Waisalamu Tanzania (Bakwata) Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Bilal Mfaume amewataka  vijana kujitambua na kufanyakazi kwa bidii kwa kuwa ndio chachu ya maendeleo kiuchumi na kisiasa.

Mfaume ameyasema hayo alipokuwa akizungumza kwenye semina ya siku moja iliyohudisha vijana wa kiislamu na baadhi ya viongozi wao.

“Vijana mna nafasi kubwa katika jamii hivyo ni vyema mkatumia umri wenu huu kufanya kazi kwa bidii kwani ninyi ndio chachu ya maendeleo katika sekta zote muhimu ikiwemo uchumi na siasa,”.

“Ninawashauri hivyo kwasababu uislamu unatambua kwamba vijana ni rasilimali katika imani na wakiandaliwa vizuri basi umeandaa nguvu kazi ya kuendeleza uislamu na taifa,”.

“Katika semina hii vijana wanafundishwa ili wajue nafasi yao katika jamii na sio tu ndani  ya uislamu peke yake kwani wao wanachanganyika na makundi mengine ya vijana wasiokuwa waislamu,” amesema Mfaume.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa jumuiya ya vijana wa kiislamu (Bakwata) Mkoa wa Kilimanjaro, Idris Muro amesema semina hiyo ni muhimu kwa vijana wa kiislamu kwakuwa itawajengea uwezo wa kutambua majukumu yao katika jamii.

“Tunawaomba mafundisho mtakayopata hapa mkayatumie vizuri katika jamii inayowazunguka na pia muweze kushiriki vyema katika chaguzi zinazokuja ikiwemo za serikali ya mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu” amesema. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles