23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli awacharukia wanaowapa mimba wanafunzi Rukwa

Anna Potinus

Rais John Magufuli amewataka wakazi wa Mkoa wa Rukwa kuacha tabia ya kuwapa ujauzito wanafunzi na badala yake kutafuta watu ambao wameshamaliza shule.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Oktoba 7, alipokuwa akizungumza na wananchi katika uwanja wa Mandela baada ya kuzindua mradi wa maji safi na mazingira na Msikiti wa Istiqaama uliopo eneo la Majengo mkoani humo.

“Kwa takwimu nilizo nazo Mkoa wa Rukwa ni miongo mwa mikoa inayowapa wanafunzi ujauzito, nimeambiwa kwa mwaka jana tu wanafunzi 229 walipata ujauzito, tumeeleza tumekua ukitoa fedha kwaajili ya elimu bure kwa watoto wetu ninyi mnatoa mimba bure sasa tutakuwa tunatoa hela kumbe tunapata hasara,”

“Ninajua mnakula vyakula vyenye nguvu mkatafute ambao wamemaliza muda wao, msiwaonee hawa wanafunzi na nyie watoto muache viherehere mtayakuta tu baadae kwahiyo hili ni lazima tulisimamie na nyie wazazi tuwafundishe watoto wetu yani unamuona kila siku anaenda kusoma hata daftari hana na unamuacha tu,”

“Hawa ni watoto masikini tusiwarubuni kwakuwa ni malaika na vyombo vya dola muanze kuwashughulikia hawa watu wanaowapa mimba kwani sheria inajulikana ni miaka 30 akishaenda gerezani ataelewa nini maana ya mimba, hii ni aibu kubwa katika mkoa wenu,” amesema.

Aidha amesemakuwa inasikitisha kuona Mkoa wa Rukwa ambao ni wa pili kwa kuzalisha mazao ndio unaoongoza kwa kuwapa mimba watoto, na hivyo akawataka waachane na tabia hiyo na ile ya kuwozesha watoto wakiwa wadogo na badala yake wawaache wamalize masomo yao kwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles