30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

TRA yakamata makontena tisa Dar

Pg 1 mbiliNA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukamata makontena tisa, mali ya Kampuni ya Heritage Limited yakiwa katika eneo la maficho ya Mbezi Tangi bovu, Dar es Salaam kinyume cha sheria.

Akizungumza kuhusu ukamataji huo akiwa eneo la tukio jana, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi TRA, Richard Kayombo, alisema taarifa hizo walipewa na msamaria mwema.

“Taarifa za kukamata makontena hayo tulipewa na msamaria mwema aliyetuambia kwamba usafirishaji ulifanyika jana (juzi) usiku kutoka bandari kavu ya PMM iliyopo Vingunguti na kibali cha bandarini kilikuwa cha Septemba 17, mwaka huu, hivyo kilikuwa kimeisha muda wake,” alisema Kayombo.

Mkurugenzi huyo alisema kwa mujibu wa nyaraka ya bandari, inaonyesha mzigo huo ulipaswa kwenda Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji Bidhaa ya Kuuza Nje (EPZ), lakini katika hali ya kushangaza ulikamatwa ukiwa Mbezi Tangi bovu kinyume na taratibu.

“Taarifa za makontena hayo zinaonyesha mwenye makontena ni Kampuni ya Heritage Limited iliyo na Tin namba 1165536501 na wakala wa forodha wa mzigo huo ni Kampuni ya Nipoc Africa Limited yenye Tin namba 105595387,” alisema Kayombo.

Alisema baada ya kupata taarifa hiyo kutoka kwa msamaria mwema, mzigo huo ulikamatwa jana na kikosi maalumu cha TRA kinachojulikana kama ‘Fast Team’ kwa kushirikiana na askari wa Jeshi la Polisi.

Kayombo alisema TRA kwa mujibu wa sheria wanatakiwa kumtafuta wakala wa mzigo huo na kama hatatokea kwa muda wa saa 24 kuanzia jana, wanaruhusiwa kufungua kontena hizo na kuangalia bidhaa zilizomo.

“Kama hatajitokeza hadi kesho (leo), tutafungua makontena na kuona bidhaa ambazo zimebebwa, kama zitakuwa halali zitataifishwa na kuuzwa, na kama zitakuwa haramu zitateketezwa kwa mujibu wa sheria,” alisema Kayombo.

Mkurugenzi huyo alisema kwamba katika hatua ya awali wamebaini mmiliki wa eneo hilo la Mbezi Tangi bovu ambalo si rasmi, ndiye mmiliki wa bandari kavu ya PMM iliyopo Vingunguti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles