28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Hospitali ya rufaa Kilimanjaro yakabiliwa na uhaba wa watumishi, madaktari

Safina Sarwatt- Moshi

HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi, inakabiliwa na upungufu wa watumishi 232 wa kada mbalimbali kulingana na ikama ya watumishi hospitali ya rufaa, madaktari bingwa 14, maofisa wauguzi wasaidizi 33 na wauguzi 95.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Josephine Rogath, alisema hayo wakati wa zaira ya Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT), Thuwaybah Kissasi, alipotembelea wodi ya kinamama wajawazito na waliojifungua hospitalini hapo.

Dk. Josephine alisema, hospitali hiyo kongwe ambayo ilianza kujengwa kama zahanati ya kutibu askari wa Kijerumani mwaka 1920, kwa sasa ina watumishi 449 wa kada mbalimbali.

Alisema hospitali hiyo haina kabisa madaktari bingwa wa dawa za usingizi, Ofisa utumishi na wataalam wa kada za wahudumu wa afya katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Alisema changamoto nyingine wanayokabiliana nayo ni ukosefu wa uzio kuzunguka hospitali hiyo hali inayosababisha kukosekana kwa usalama wa wagonjwa, watumishi na mali za hospitali.

 “Uchakavu wa miundombinu ya hospitali ikiwemo wodi na majengo mbalimbali ni changamoto nyingine inayotukabili pamoja na ukosefu wa vifaa tiba kama vifaa vya mionzi (ultrasound), CT Scan, ECG pamoja na ukosefu wa vifaa kwa ajili ya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU)” alisema Dk. Josephine.

Kwa upande wake, Kissasi aliyeongozana na Katibu mkuu wa umoja huo, Mwalimu Queen Mlozi, aliwatia moyo watumishi wa hospitali hiyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii japo licha ya kuwepo kwa changamoto hizo.

Alisema dhamira ya Serikali ya awamu ya tano ni kuwatumikia wananchi bila kujali itikadi ya chama wala dini na kuwataka kila mmoja kuhakikisha anatimiza majukumu yake.

Aidha alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli kwa kutekeleza ilani kwa vitendo na kuwataka kuzidi kumuombea na kuwafichua wale wote wanaokwamisha utekelezaji wa ilani.

Mbali na viongozi hao kutembelea hiyo, walifanya usafi katika soko la Mbuyuni ambapo kilele cha kongamano  la kumpongeza Rais Magufuli kwa kutekeleza ilani kwa vitendo linatafanyika leo katika viwanja vya Majengo Manispaa ya Moshi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles