27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

Ngariba mstaafu adai kupewa talaka kwasababu amekeketwa

Dotto Mwaibale- Singida

NGARIBA mstaafu, Hawa Njolo, mkazi wa Kijiji cha Sagara Wilaya ya Singida amedai mme wake amempa takala kwasababu amekeketwa.

Alitoa ushuhuda wake huo mbele ya wanawake wenzake waliohudhuria kliniki katika  Kijiji cha Mughamo iliyoandaliwa na Shirika la Empower Society Transform Lives (ESTL).

Alisema wakati akiishi na mume wake Babati mjini Mkoa wa Manyara, mume wake alianza tabia ya kutembea nje ya ndoa na mwanamke ambaye hakukeketwa.

“Habari hizo nilizipata kwa wasiri wangu na hakuchukua muda akawa ananifanyia vituko mara kwa mara, alipoona hakuna dalili ya kuachana naye alinilima talaka,”

“Binafsi nilikuwa namheshimu sana mume wangu na ndugu zake, nilikuwa msafi na mapishi nilikuwa vizuri wala sikuwa mwanamke wa magenge, lakini bado nikapewa takala,” alisema Njolo.

Alisema mume wake alimuacha akidai kwasababu amekeketwa hasikii raha wakati wa tendo la ndoa.

Ngariba huyo ambaye alirithi kazi hiyo kutoka kwa bibi yake, alitoa ushuhuda huo ikiwa ni sehemu ya elimu  juu ya madhara ya ukeketaji aliyokuwa akiitoa kwa baadhi ya wanawake waliohudhuria  kliniki hiyo.

Mkazi mwingine wa Kijiji cha Mughamo Zanura Maulidi, alisema yeye pia ni mwaathirika wa kukeketwa.

 ‘Mwaka 2011 tulifunga ndoa na mume wangu (hakumtaja jina) na tukiwa katika ndoa kwa  miaka nane, mwenzangu alioa mke wa pili ambaye hajakeketwa na mume wangu anadai anamvutia wakati wa tendo la ndoa kuliko mimi,” alisema.

Zanura aliomba mafunzo hayo yatolewe pia kwa wanaume ili kupunguza kasi ya kuachwa wanawake waliokeketwa.

Kaimu Meneja wa ESTL, Philbert Swai, alisema mradi huo unafadhiliwa na The Foundation for civil society kwa Sh milioni 60 kwa mwaka moja na malengo yake ni kushirikisha makundi mbalimbali ya kijamii kubuni njia za kudumu kukomesha ukeketaji na ukatili wa kinjisia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,404FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles