27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi wakiri kumshikilia mwandishi wa habari

Francis Godwin – Iringa

JESHI la  polisi  Mkoa  wa Iringa limesema limemkamata  Mhariri wa Uzalishaji Maudhui na Msimamizi Msaidizi wa Watetezi TV, Joseph Gandye, ili awaonyeshe askari  waliohusika kusimamia watuhumiwa wa wizi kulawitiana wakati wakiwa mahabusu katika Kituo cha Polisi Mafinga.

 Akizungumza na mwandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire, alisema mwanahabari  huyo alikamatwa jana jijini Dar es Salaam na kuwekwa katika Kituo cha Polisi cha Urafiki kabla ya kusafirishwa  kwenda mkoani Iringa.

“Tumemkamaa huyu mwandishi Joseph Gandye badala ya kujibizana kwenye mitandao tunataka aje huku Iringa ili akatuonyeshe na kuthibitisha habari alizoziandika na  kuzisambaza mitandaoni kuwa kuna watuhumiwa  walilazimishwa kuingiliana kinyume na maumbile  wakiwa kituo cha Polisi Mafinga  wilayani Mufindi.

 “Hatuzuii taratibu nyingine za kwao ama ndugu kwa ajili ya dhamana na kuja na wakili wake kumsikiliza ila sisi  tupo kwenye uchunguzi wetu kwa kumkamaa  mwandishi  aliyeandika ili ikibainika ukweli sheria ichukue hatua zake, “alisema Bwire.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari aliyoitoa Agosti 14,  Kamanda Bwire alisema mtuhumiwa Ambrose  Malya (35) alidai kulazimishwa kuingiliana kinyume na maumbile akiwa mahabusu, suala alilolifikisha ofisini kwake na polisi ilianza uchunguzi .

 “Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa kwenye mitandao  ya kijamii kuhusu kudhalilishwa  kwa  watuhumiwa  kwenye kituo cha Polisi cha Mafinga wilaya ya Mufindi.

“Malalamiko hayo yanatokana na kesi ya msingi  iliyoripotiwa kituo cha polisi Mei 5 kwa jalada namba MFG/RB/1302/2019  kosa la wizi wa mafuta ya Dieseli, mota na mashine ya kuchoma vyuma kwenye kiwanda  cha Hongwei International Company Ltd cha Mafinga  na kupelekea  watuhumiwa sita kukamatwa  na kuhojiwa  na polisi”ilisema ya Bwire.

Ilisema Malya ni miongoni mwa watuhumiwa sita  waliokamatwa kwa hizo za wizi .

 “Mara baada ya kupata taarifa hizo kama kamanda wa  Polisi nilimuagiza Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai Issa J . Sulleiman – ACP kufungua jalada na kuanza  upelelezi wa haraka sana ambapo alitekeleza  maagizo hayo na kufungua jarada namba IRR/CID/PE/31/2019”  ilisema.

Taarifa ilisema upelelezi ulibaini madai hayo si ya kweli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles