27.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 20, 2023

Contact us: [email protected]

Vifo ajali ya lori la mafuta vyafika 101

Aveline Kitomary , Dar es salaam

IDADI ya vifo vya majeruhi wa ajali ya lori la mafuta iliyotokea mkoani Morogoro, imefika 101 baada ya majeruhi mmoja aliyekuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kufariki dunia usiku wa kuamkia jana.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano MNH, Aminiel Aligaesha, alisema aliyefariki dunia ni Sadiki ismail (31).

Alisema mpaka sasa kati ya majeruhi 47 waliofikishwa hospitalini hapo, waliobaki ni 14 ambapo kati yao 11 wako katika Vyumba vya Uangalizi Maalum (ICU) na watatu wako katika wodi za kawaida na hali zao zinaendelea vizuri.

“Awali tulikuwa tumebakiwa na majeruhi 15 lakini usiku wa kuamkia leo (jana) saa kumi alfajili majeruhi mmoja Sadiki Ismail amefariki duni, kwahiyo sasa tumebakiwa na majeruhi 11 kati ya hao 11 wako ICU na watatu wapo katika wodi za kawaida za sewahaji na wanaendelea vizuri na wanafanya mazoezi,”alisema Aligaeshi.

 Alisema hakuna changamoto zilizojitokeza wakati wa upimaji wa vina saba na tayari kila majeruhi anandugu yake.

“Mpaka sasa zoezi la DNA kwa majeruhi wa ajali ya moto limefanikiwa bila dosari yoyote kila majeruhi sasa anandugu yake na wanafatilia hali zao,”alieleza Aligaesha.

Alisisitiza kuwa hospitali hiyo inavifaa na dawa za kutosha huku vingine wakipewa kutoka serikalini na kwa wadau mbalimbali ambao wanatoa misaada na kuwataka watu waendelee kujitokeza kwani  vifaa pia vinahitaji kwa matumizi ya hospitali.

“kama mtu au taasisi wanataka kutuletea msaada  hatutaacha kupokea kwasabubu tunazo sisi tutazipokea tu kwani zinahitajika kwa hositali yetu hata kama tunazo ninawasihi watu waendelee tu kutoa misaada kwaajili ya kuwasaidia watu wengine,”alisema Aligaesha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles