25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kipenga uchaguzi Serikali za Mitaa chapulizwa rasmi

Ramadhan Hassan -Dodoma

BAADA ya sintofahamu ya muda mrefu juu ya tarehe ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Serikali imetangaza Novemba 24 ndiyo siku ya uchaguzi huo ambapo viongozi wa vijiji na mitaa watapatikana.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo, jana alisema siku hiyo upigaji kura utaanza saa mbili kamili asubuhi na kumalizika saa 12 jioni.

Pia aliwaagizana wakuu wa mikoa na wilaya kuhalikisha wanasimamia shughuli zote za uchaguzi utakaohusisha vijiji 12,319 na mitaa 4,294, vitongoji 64,384 ili ziweze kufanyika kwa amani na utulivu. 

RATIBA KAMILI

Jafo alisema Septemba 2 hadi 9 itakuwa ni kwa ajili ya uteuzi wa wasimamizi wa uchaguzi ambapo Mamlaka za utezuzi zitahusika.

Alisema Septemba 13 mwaka huu ni tangazo la majina ya mipaka ya vijiji na vitongoji ambapo mhusika ni msimamizi wa uchaguzi.

Waziri Jafo alisema Septemba 22 mpaka 16 mwaka huu ni uteuzi wa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na wasimamizi wa vituo.

“Septemba 23 ni maelekezo kuhusu uchaguzi na  Oktoba 3 ikiwa ni uteuzi wa waandikishaji wa wapiga kura huku Oktoba 4 mpaka 6 ikiwa ni viapo kwa waandikishaji wa wapiga kura, wasimamizi wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi,”alisema Jafo.

Alisema Oktoba 4 hadi 6 ni kwa ajili ya elimu kwa waandikishaji wapiga kura ambapo Oktoba 8 mpaka 14 ni kwa ajili ya zoezi la uandikishaji wa wapiga kura na Oktoba 15 ikiwa ni siku ya kubandikwa kwa orodha ya wapiga kura,”alisema,

Jafo alisema Oktoba 15 mpaka 21 itakuwa ni kwa ajili ya orodha ya wapiga kura huku Oktoba ambapo itaendana na zoezi la pingamizi kuhusu uandikishaji wa wapiga kura.

Alisema Oktoba 21 mpaka 22 ni kwa kuhusu pingamizi huku pia Oktoba 21 mpaka 22 ikiwa ni kwa ajili ya orodha ya wapiga kura na Oktoba 21 hadi 26 ikiwa ni kwa ajili ya uamuzi wa rufaa.

Waziri huyo alisema Oktoba 22 mwaka huu ni kwa ajili ya kukoma uongozi kwa viongozi waliopo madarakani na Oktoba 29 ni kwa ajili ya wagombea  kuchukua fomu.

Alisema Oktoba 29 mpaka Novemba 4 ni kwa ajili ya kurejesha fomu na Oktoba 29 ni kwa ajili ya uteuzi wa kamati ya rufaa huku Novemba 5 ikiwa ni kwa ajili ya uteuzi wa wagombea.

“Tarehe 5 mpaka 6 ni kwa ajili ya uwasilishaji wa pingamizi kuhusu uteuzi wa wagombea na Novemba 5 mpaka 7 ikiwa ni uamuzi wa pingamizi kuhusu uteuzi wa wagombea.

Alisema  Novemba 5 mpaka 8 ni kukata rufaa dhidi ya uamuzi kuhusu pingamizi la uteuzi huku Novemba 5 mpaka 9 ikiwa ni uamuzi wa kukata rufaa.

Alisema Novemba 10 ni uwasilishaji wa ratiba za mikutano ya kampeni kutoka kutoka katika vyama vya siasa ambapo Novemba 14 ni uwasilishaji wa ratiba za mikutano ya kampeni kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya huku Novemba 17 mpaka 23 ikiwa ni siku za kuanza kwa kampeni.

Alisema Novemba 24 itakuwa ndio siku ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Nafasi zitakazogombewa

Jafo alisema nafasi zitakazogombewa ni Mwenyeviti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Midogo, mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wa kamati ya mtaa kundi mchanganyiko la wanaume na wanawake na wajumbe wa kamati ya mtaa kundi la wanawake katika mamlaka za miji.

Jafo alisema nafasi nyingine ni ya mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa halmashauri ya kijiji kundi mchanganyiko la wanaume na wanawake, wajumbe wa halmashauri ya kijiji kundi la wanawake na wenyeviti wa vitongoji katika mamlaka za wilaya.

Wagombea

 Jafo alisema kwa mujibu wa kanuni hizo, wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi watatakiwa kuwa wanachama na wadhamininiwa wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu

Kuhusu uchaguzi

Jafo alisema kwa mujibu wa kanuni, Msimamizi wa Uchaguzi atatoa maelekezo ya Uchaguzi siku sitini na mbili kabla ya siku ya uchaguzi.

Alisema kwa mujibu wa kanuni, Msimamizi wa Uchaguzi atafanya uteuzi wa watumishi wa ummawatakaoandikisha na kuandaa Orodha ya wapiga kura52 kabla ya siku ya uchaguzi.

Kuhusu uandikishaji wa wapiga kura, Jafo alisema kwa mujibu wa kanuni hizo, uandikishaji na uandaaji wa orodha ya wapiga kura utaanza siku 47 kabla ya siku ya uchaguzi na utafanyika kwa muda wa siku saba.

“Kwa mujibu wa kanuni hizo, vituo vya kujiandikisha kupiga kura na kupigia kura, kwa maeneo yaliyo chini ya halmashauri za wilaya na mamlaka za miji midogo vitakuwa katika ngazi ya kitongoji.

“Kwa upande wa mamlaka za miji, vituo vya kujiandikisha kupiga kura na kupigia kura vitakuwa katika ngazi ya mtaa,”alisema Jafo.

Muda wa kuchukua na kurejesha fomu

Jafo alisemakwa mujibu wa kanuni hizo, mtu yeyote anayekusudia kugombea nafasi za uongozi, atatakiwa kuchukua fomu ya uteuzi wa kugombea nafasi husika siku zisizopungua 26 kabla ya siku ya uchaguzi.

“Kwa kadri itakavyoelekezwa na msimamizi wa uchaguzi na kutakiwa kurejesha fomu husika ndani ya muda wa siku saba tangu siku ya kwanza ya uchukuaji wa fomu iliyotangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi,”alisema Jafo.

 Utaratibu wa uteuzi

Alisema kwa kujibu wa kanuni hizo, msimamizi msaidizi wa uchaguzi atafanya uteuzi wa wagombea wa nafasi zilizoainishwa katika kanuni hizi, kabla ya tarehe ya uchaguzi kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa 12 jioni.

Endapo wagombea hawataridhika na maamuzi ya msimamizi au msimamizi msaidizi wa uchaguzi kuhusu uteuzi wa wagombea, kutakuwa na kamati ya rufani katika kila wilaya ambayo itasikiliza mapingamizi kuhusu uteuzi wa wagombea katika wilaya husika. Wajumbe wa kamati ya rufani watateuliwasiku saba kabla ya siku ya uteuzi wa wagombea,”alisema  

Kuhusiana na waangalizi alisema kwa mujibu wa kanuni hizo, wataruhusiwa kuangalia uchaguzi baada ya kupata kibali cha katibu mkuu wa wizara yenye dhamana ya serikali za mitaa.

Kampeni

Jafo alisema kwa mujibu wa kanuni hizi, kampeni za uchaguzi zitafanyika siku 7 kabla ya siku ya Uchaguzi.

Aidha, Kanuni zinaelekeza, kila Chama cha Siasa kinachoshiriki Uchaguzi kitawasilisha ratiba yake ya mikutano ya kampeni ya Uchaguzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi si chini ya siku saba kabla ya kuanza kwa kampeni.

MAONI YA VYAMA VYA SIASA

Akitoa maoni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Salum Mwalimu alilaani kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi kwamba wapo tayari kusimamia uchaguzi na kwamba hapa ni kazi tu.

Dk. Nchimbi alitoa kauli hiyo wakati alipopewa nafasi ya kutoa neno la shukrani kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa.

“Kauli ya kwamba wamejipanga na wanaenda kushinda ni kielezo cha kuonesha kwamba haki haitakuwepo, Hatujatoka hapa tayari hali ya hewa imeanza kubadilika unaona kauli ya Mkuu wa Mkoa hapa kazi tu hatuna sababu ya kutuambia haya.

“Wapo wakuu wa mikoa walisema shughuli itaonekasna katika uchaguzi wa serikali za mitaa tunawaambia kama wamejiandaa kwa uchuguzi sawana kama wamejiandaa kwa uchafuzi tutakutana katika uchaguzi.

Naibu Katibu Mkuu huyo alisema Chadema watasimamisha wagombea katika kila sehemu ya nchi na wala hawatamuogopa mtu  

CCM

Kwa upande wake, Naibu katibu Mkuu CCM, Zanzibar, Dk.Abdallah, Juma Sadala, alisema CCM wapo tayari kwa uchaguzi huo huku akidai kwamba wale wanaolalamika Demokrasia wanakosea kwani ipo vizuri.

Alisema maoni ya vyama vya siasa yameingizwa katika kanuni na mwongozo wa uchaguzi wa serikali za mitaa na wala hakuna haja ya baadhi ya vyama kuanza kulalamika.

SHIBUDA

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Vyama vya siasa nchini, John Shibuda, alisema kanuni na mwongozo wa uchaguzi wa Serikali za mitaa bado hajazipitia lakini kuna haja ya vyama kuungana ili kushindana na CCM.

“Sijazisoma bado ngoja nizisome ila zinahitajika nguvu za ziada kushindana na CCM,”alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles