28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

TRA: Mfanyabiasha ana haki ya kupata taarifa za kodi

KOKU DAVID-DAR ES SALAAM

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imesema mfanyabiashara ana haki ya kupata taarifa zinazohusiana na kodi, mabadiliko ya sheria za kodi, tozo na ada mbalimbali anazotakiwa kulipa.

Akizungumza jijini Dar es Salam, Meneja wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Diana Masala, amesema kuwa pamoja na kujua haki zake anatakiwa kupata elimu ya mara kwa mara itakayomuwezesha kuwa na utayari wa kulipa kodi kwa hiyari.

Amesema katika kuelekea uchumi wa kati wa viwanda serikali imepunguza baadhi ya kodi ili kuvutia wawekezaji  na kwamba punguzo hilo litahusu wawekezaji wote wa ndani na nje.

Amesema kwa upande wa wafanyabiashara binafsi, kodi ya mapato hutozwa kutokana na mauzo yao na kwamba katika mwaka wa fedha wa 2019/20 viwango vya kodi vimepunguzwa na kwa mfanyabiashara binafsi atakayekuwa ametunza kumbukumbu zake atanufaika zaidi na punguzo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles