MWIGIZAJI wa siku nyingi nchini, Susan Humba ‘Natasha’, amesema wazalishaji wa filamu wengi wa Tanzania walikuwa wakitumia majina ya Kiingereza kwenye filamu zao kwa madai kwamba huvutia yanapotamkwa tofauti na ya Kiswahili.
“Wazalishaji wa filamu hizo walikuwa wakidai kwamba majina hayo huvutia kutamkwa mfano ‘My love’, inavuta na inatamkika vema kuliko ‘Mpenzi wangu’.
Hata hivyo, alieleza kwamba miaka ya sasa wengi wamebadilisha hulka hiyo na kutumia majina ya Kiswahili yenye maana husika wa matukio yaliyopo katika filamu zao na yanafanya vema sokoni.
“Mkiangalia kwa miaka ya sasa mambo hayo yanaonekana kupotea na waandaaji wengi wameelimika wanatumia majina mengi ya Kiswahili na yanaonyesha kufanya vizuri hivyo kuua hulka kwamba majina ya Kiingereza tu ndiyo yenye soko yanapowekwa katika ‘kava’ za filamu za kibongo,” alimaliza.