30.4 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Kamwelwe awatolea uvivu wanasiasa wanaongilia zabuni za ujenzi

Anna Potinus – Dar es Salaam

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isaac Kamwelwe, amewajia juu wanasiasa wanaoingilia masuala ya uchambuzi wa zabuni ambapo amewataka kuachana na tabia hiyo na kuipa nafasi serikali kfanya kazi yake.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Julai 29, wakati akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi la urefu wa kilomita 3.2 katika ziwa Victoria litakalojengwa kwa muda wa miezi 48.

“Huu mkataba wa Kigongo-Busisi nikiwaambia yaliyotekea ni maajabu, sasa hivi inakua ni tabia tenda ikishatangazwa watu wanaanza kujipanga kumwambia mkandarasi ili wapate hela hiyo ni tabia chafu tena wengine ni viongozi kama mimi na bahati nzuri hawaji kwangu kwasababu wataambulia matusi,” amesema.

“Tenda zikishatangazwa kuna watu wanaanza kujiendekeza, mimi ninasema hata angekuwa ni mtoto wangu ukiniletea hilo siku hiyo na nyumbani kwangu unahama, sasa niwaombe wale ambao walizoea kule tulikotoka kila tenda ikitangazwa wanaanza kupitapita waache serikali ifanye kazi yake ili wakikosea taratibu zipo tuwafunge,” amesema.

 “Wengine ninawaheshimu lakini wanataka kuingilia masuala ya uchambuzi wa tenda, jamani sio kazi ya wanasiasa tuachie serikali ifanye kazi yake, huyu Mfugale anapambana na mengi wengine hawana aibu wanampigia simu, wanamuandikia barua na wengine wanamshtaki kwenye Taasisi za serikali, hatuendi hivyo uliza kwanza unachotaka kufanya,” amesema.

Aidha amesema daraja hilo la Kigongo-Busisi linalotarajia kugharimu bilioni 592, litaunganisha vema nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa usafiri wa ardhini na hivyo kupunguza muda wa kusafiri na kuleta tija katika kufanya biashara miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles