Mwandishi Wetu, Simiyu
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), inatarajia kushiriki kwenye maadhimisho ya sherehe za Maonesho ya Wakulima (Nanenane) ambayo kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu kuanzia Julai 28 Agosti 10, mwaka huu.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Peter Ngamilo amesema katika maadhimisho hayo, TAEC itaonesha shughuli mbalimbali zinazofanywa na tume hiyo ikiwamo utoaji wa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali juu ya udhibiti na matumizi salama ya mionzi nchini.
“Aidha, elimu kwa wananchi juu ya matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia kwenye sekta za afya, kilimo, viwanda, mifugo, maji, lishe pamoja na ujenzi itatolewa kwenye banda letu katika maonesho hayo.
“Wananchi wote wanakaribishwa ili kujipatia elimu bure kwa njia za maelezo, video fupi, vipeperushi na majarida ili kujiongezea uelewa juu ya majukumu yanayotekelezwa kisheria na TAEC katika nyanja za udhibiti wa mionzi na uhamasishaji wa matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia,” amesema amesema Ngamilo.