32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Bibi wa miaka 83 apatikana na hatia ya bangi Kenya

NAIROBI –KENYA

Mwanamke mmoja mwenye miaka 83 aliyekutwa na gramu 600 za bangi amekutwa na hatia nchini Kenya.

Taarifa zilizoripotiwa na Kituo cha Redio cha Capital fm  cha nchini Kenya zinaeleza kuwa mwanamke huyo alitiwa hatiani jana mbele ya Hakimu Mkazi Nelly Kariuki.

Akiwa mbele ya hakimu Kariuki jana, Lydia Mumbi Ndirangu alikiri kuwa alikutwa na bangi ya thamani ya shilingi za Kenya 500 sawa na shilingi za Kitanzania 12,000  katika eneo la Muthinga, jimbo la Tetu.

Mtuhumiwa ataendelea kushikiliwa na  atatakiwa kurudi tena mahakamani Julai 15 mwaka huu wakati atakaposomewa hukumu.

Kesi inayomkabili bibi hiyo ni ya pili ikihusiana na bangi katika kipindi cha miezi miwili tu nchini Kenya.

Mwezi Mei mwaka huu, Mahakama ya Nyeri ilimhukumu mwanamke mmoja wa makamo, kifungo cha miaka 30 bila faini kwa makosa ya kusafirisha bangi ya thamani ya shilingi za Kenya 2,820  ambazo ni sawa na shilingi za Tanzania 63,000.

Gazeti la daily Nation la nchini Kenya limeandika kuwa inaaminika bibi huyo amekuwa akinunua bangi  mjini Nyeri na kuipeleka kwa mtoto wake wa kiume ambaye huwauzia wateja.

Mei 2019 ilitoka ripoti inayoonyesha kuwa Tanzania na Kenya zinaongoza kwa uvutaji wa bangi Afrika mashariki.

Kulingana na utafiti wa watumizi wa marijuana uliofanywa na shirika la New Frontier Data kutoka Uingereza, Tanzania ambayo iko katika nafasi ya tano kwa idadi ya watumiaji wa mmea huo barani Afrika, inaongoza eneo la Afrika mashariki ikiwa na watu milioni 3.6 wanaotumia bangi ikifuatiwa na Kenya ambayo iko nafasi ya sita na watu milioni 3.3 na Uganda katika nafasi ya nane ikiwa na watumiaji milioni 2.6.

Ripoti hiyo iliyataja mataifa yanayoongoza kwa uvutaji wa bangi barani Afrika ni Nigeria iliyo na watumiaji milioni 20.8, ikifuatiwa na Ethiopia yenye watu milioni 7.1, Misri watu milioni 5.9 huku taifa la Kongo likiwa la 4 na watu milioni 5.

Mataifa ya Burundi na Sudan Kusini hayakuorodheshwa.

Lakini taifa la Sudan linashikilia nafasi ya 7, ilikiwa na watumizi milioni 2.7, likifuatiwa na Madagascar lenye watu milioni 2.1, Ghana milioni 2, Msumbiji watu milioni 1.9, na Angola watu milioni 1.8.

Mataifa ya Afrika yalio na watumizi wa wachache wa bangi kulingana na ripoti hiyo ya 2019 ni pamoja na Zimbabwe iliyo na watu milioni 1.1, Malawi watu milioni 1.2, Niger watu milioni 1.2 na Zambia watu milioni 1.4

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles