25.1 C
Dar es Salaam
Monday, October 28, 2024

Contact us: [email protected]

Ruksa kisheria kumuacha mwenza aliye gerezani muda mrefu

KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

SUALA la ndoa kiujumla wake linagusa watu wote na huwezi kuanza kuzungumzia yatokanayo kwenye ndoa kama hujaanza kueleza nini maana yake.

Hivyo ndivyo alivyoanza Wakili Maarufu nchini, Twaha Taslima, katika mahojiano maalum na MTANZANIA kuhusu migogoro ya ndoa, talaka nabchangamoto zilizopo ndani yake.

Taslima anasema katika Sheria ya Ndoa ya mwaka 1977, kifungu namba tisa kinaeleza maana ya ndoa kuwa ni muungano wa hiari wa mwanamume na mwanamke, wenye nia ya kuishi pamoja katika muda wote wa maishamyao.

Anasema kuna ndoa ya kidini, kiserikali ambazo zina cheti cha ndoa na ya kimila ambayo haina cheti cha ndoa kisheria.

“Kuna ndoa za aina mbili, mke mmoja na ya mke zaidi ya mmoja.

Sheria inaruhusu kubadilisha mfumo wa ndoa wakati wahusika wako ndaniya ndoa. Kwa mfano, kutoka mfumo wa mke mmoja kuwa wake zaidi ya mmoja au mke zaidi ya mmoja kuwa mke mmoja,” anasema.

Twaha Taslima, akiwa na mwandishi wa makala haya

Swali: Sababu zipi za msingi zinazoweza kuvunja ama kuvunjwa kwa ndoa.

Jibu: Katika sheria hiyo ya ndoa kifungu namba 12 kinaeleza sababu ya ndoa kuvunjika ambayo ni kifo, mmoja wao anapofariki dunia, ndoa hiyo inakuwa imevunjika.

Kama kuna amri ya mahakama ya kwamba mume au mke haonekani nyumbani,

hakuna mawasiliano ya mahali alipo kwa kipindi kirefu, mmoja wao aliyeachwa nyumbani anaweza kwenda mahakamani kuomba talaka.

Mahakama itasikiliza hoja za mhusika endapo itaona kuna dhana ya kifo, basi ndoa hiyo itavunjika kwa amri ya mahakama.

Sababu nyingine mahakama inaweza kubatilisha ndoa, hii sio kuvunja bali ni kuibatilisha. Kwanini nasema

kubatilisha; endapo itabainika kuna udanganyifu wakati wa makuabaliano ya kufunga ndoa ama akatokea mmoja akashindwa kutimiza majukumu ya kindoa mara baada ya ndoa hiyo kufungwa.

Pia mahakama inaweza kuvunja ndoa pale ambapo kuna sababu kati ya wanandoa wawili zinazoonesha hiyo ndoa imevunjika na hairekebishiki.

Swali: Mume ama mke akihukumiwa

kwenda jela miaka zaidi ya mitano, ama yuko mahabusu kwa muda mrefu, uhai wa ndoa hapo ukoje?

Jibu: Kama mtu kafungwa miaka 30 kibinadamu ni ngumu kuvumili mhusika akiomba mahakamani kuvunja ndoa anaweza kupata talaka.

Swali: Endapo mume ametoka jela akakuta mkewe amezaa na mwanamume mwingine na kabla hapakuwapo na talaka anaweza kufungua madai?

Jibu: Mazingira hayo mume anaweza kudai fidia ya ugoni. Wenzetu Wasukuma

aliyeshikwa ugoni anatoa idadi fulani ya ng’ombe kama adhabu.

Adhabu hiyo ikitolewa mume ndio anaweza kuamua kama aendelee kuishi

na mkewe ama amuache.

Kwa dini ya Kiislamu zipo namna ambazo zinaangaliwa ikiwamo muda mrefu kupita bila mke na mume kugusana kimwili kama ni mke anakuwa si mke, hivyo ukihitaji kuendelea naye lazima umuoe kwa mara nyinyine.

Swali: Je, mke au mume anaweza kudai fidia kwa Serikali endapo atakaa mahabusu muda mrefu, akatoka kwa kuwa hana hatia na akakuta mkewe kaolewa na mume mwingine

Jibu: Kinachofanya talaka iwepo ni kutokuwapo kwa muhusika haijalishi ulitiwa hatiani ama uliachiwa hukuwa na hatia.

Hata kama ulituhumiwa si mkosaji, kutokuwapo kwako kwa kipindi kirefu mwenza wako anaweza kuomba talaka akapata nawe huwezi kudai fidia.

Swali: Kuna ndoa nyingi zinavunjika baada ya mke au mume kutoka gerezani na zingine zinavunjika hata kabla mhusika hajatoka anatoa talaka akiwa huko huko, nini tatizo?

Jibu: Najua ndoa nyingi zimevunjika katika mazingira hayo, lakini kikubwa ni taarifa za uongo zinazokwenda gerezani zinasababisha kuvunjika kwake.

Watu wanapeleka taarifa mbaya kuhusu mke ama mume aliyekuwa nje na kwa kuwa huoni unasikia na kuziamini ukitoka unavunja ndoa bila kujipa muda wa kutafuta ukweli.

Kikubwa katika ndoa ni kila mmoja kutimiza majukumu yake ya kindoa, mume ahudumie familia yake, ikiwa mwanamke ana uwezo anaweza kushiriki kutoa huduma na kufarijiana ili kuifanya ndoa iwe nzuri kwani kama hakuna faraja ndoa lazima iyumbe.

Wakili Taslima anamalizia kuzungumza hayo huku akieleza uzoefu wake wa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 40.

Anasema ili watu waweze kuingia katika ndoa lazima yawepo mambo yanayowavutia miongoni mweo na sababu hiyo iliyomfanya mume kuoa angependa iendelee kuwapo maisha yote.

Taslima anasema mwenza kumwelewa mwenzake wanapokuwa katika mazungumzo ama masuala yanayohusu maisha kunaifanya ndoa kudumu kwa muda mrefu.Wanandoa wanatakiwa wawe wenye kuhurumiana, wasiingize watu wa nje katika masuala yao ya kindoa ila kama inabidi kufanya hivyo.

“Katika miaka 41 ya ndoa yangu ni mara moja niliweza kushirikisha watu wa nje masuala yanayohusu ndoa yangu,”anasema.

Anasema katika ndoa kuna changamoto nyingi zinazoitikisa, ikiwamo mmoja wa wanandoa anaposhindwa kumwelewa mwenzake, anapokuwa hayuko tayari kusikiliza, kama mmoja ametoka katika tamaduni zisizofanana, mnapotoa masuala ya ndoa nje na kuishi bila hofu ya Mungu.

Wakili Taslima anasema teknolojia pia ni changamoto hasa katika matumizi ya simu, kunapokuwapo kutokuheshimiana na kufatiliana katika mazungumzo ya simu.

Anatolea mfano kwamba anaweza kuwa anazungumza kwa simu na mtu, mke hajui anazungumza na nani na hasikii kinachozungumzwa bali anasikia majibu ya sawa… muda ule ule, baada ya hapo unaibuka ugomvi akidhani ni simu ya mapenzi.

Kuangalia filamu pia kunaweza kuibua ugomvi hasa kama filamu hiyo itagusa sehemu fulani ya tofauti mliyonayo ndani ya ndoa, ugomvi unaweza kuanza mkiwa katika kuangalia hiyo filamu.

Taslima anatoa ushauri ili kuzinusuru ndoa zinazoweza kuvunjika bila sababu za msingi  anasema kila mtu afahamu umuhimu wa ndoa.

“Ili kuwa na taifa bora lazima uongozi uanzie katika familia, ndoa nzuri ndiyo inayoleta familia nzuri, kuepuka mashindano baina ya mke na mume labda katika matendo yanayoleta tija kwa wote.

“Ni vyema jamii ya Tanzania kupitia Serikali ikajitahidi kuwapa fursa wanaopanga kufunga ndoa ya kuelimishwa juu ya majukumu yao kindoa.

“Njia za kuwaelimisha wanandoa ziimarishwe ili wahusika waingie kwenye ndoa akiwa anajua cha kufanya,”anasema.

Mwanandoa Bahati Raphael (sio jina rasmi) aliyeachwa baada mumewe kutoka jela anasimulia haya:

“Mume wangu alihukumiwa kifungo cha miaka mitano kwa makosa ya wizi, lakini kwa kipindi chote nilikuwa naenda gerezani Ukonga kumtembelea.

“Nilikuwa naenda Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kabla hajahukumiwa kifungo, huku yeye akitokea mahabusu, lakini alikuwa haishi kulalamika.

“Alikuwa akinituhumu kuwa na wanaume, tulikuwa tunagombana na wakati mwingine

nikipeleka chakula gerezani anagoma kupokea,” anasimulia na kuongeza:

“Alitoka gerezani mwaka jana, alifika nyumbani nilifurahi mno, lakini huwezi amini furaha yangu ilidumu kwa wiki moja tu na wiki ya pili aliamua kuniacha.

“Ndani ya wiki moja yalitawala malalamiko kwamba nimebadilika, lakini hata mimi niliona

mume wangu kabadilika kitabia.

“Kuna masuala ya kindoa tuliyokuwa tunashiriki aliporudi alitaka kubadili mfumo, lakini

nilipohoji na kukataa kufanya anachotaka kufanya alisema alikuwa ananipima aone kama naweza kukubali kwa sababu kanikuta nimebadilika.”

Anasema kuanzia hapo hakunifurahia tena na ilipofika wiki ya pili alitoka kwenda kwa

marafiki zake na aliporudi alirudi na talaka mkononi huku akiwa ameambatana na mashahidi wake, akamkabidhi talaka na sasa yuko kweo Chamazi.

Anawashauri wanandoa waheshimiane na kuaminiana kwani imani inapotoweka ndoa huvunjika.

“Wale wanaofuatilia ndoa za wenzao waache kufanya hivyo, kwani taarifa zikiwa za uongo

zinaumiza na kusababisha ndoa kuvunjika.”

Justine Exavery anasema aliwahi kuwa na kesi ya jinai, alituhumiwa kwa udanganyifu

lakini kesi ilichukua miaka mitatu ikaisha akaachiwa huru.

Anasema wanawake wanapitia wakati mgumu hasa pindi waume zao wanapofikwa na kesi kwani katika kipindi cha kutafuta msaada wa nini afanye ili mumewe atoke katika hiyo kesi, anakutana na wenye kutoa msaada kwa nia njema na wale wanaotoa msaada kisha wanaomba uhusiano wa kimapenzi na mwanamke.

Mwanamke akiangalia matatizo aliyonayo na shida yake kubwa mumewe atoke jela ama amalizekesi inayomkabili, basi hukubali kila anachoelekezwa kufanya na watoa msaada.

“Watu si wazuri kabisa, ukipata tatizo badala ya kukuhurumia anatumia nafasi hiyo kuchukua mkeo ama kumuingiza katika kuisaliti ndoa yake, lakini

yote anafanya kwa kulazimishwa, si hiari yake.

“Mwanamke jasiri hupambana na hizo changamoto, hakubali kuingia katika huo mtego na wakati mwingine Mungu anamsaidia anafanikiwa.

“Baadhi ya watu wako kwa ajili ya kuchukua wake wa wenzao wanapokuwa na shida, hili hasa ndilo linaloleta mgogoro kwenye ndoa na kama hufikirii sawa sawa unavunja ndoa,” anasema Justine.

Akizungumzia kwa upande wa wanaume anasema wao mke akiwa kwenye matatizo kama hayo huwa hawashawishiwi bali huchepuka wenyewe bila kulazimishwa.

Justine anasema wapambe ni hatari, wanashiriki katika usaliti lakini baadae wanabadilika, hao hao ndio wanaofikisha taarifa kwa mlengwa kuhusu usaliti unaofanyika kwa lengo la kuvuruga

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles