26.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

M-Pawa yazawadia washindi wa droo ya 3, watumiaji wafikia milioni 8.5

Mwandishi wetu

Benki ya CBA na Vodacom leo Juni 27, wametangaza washindi wa droo ya tatu kwa ajili ya promosheni yao ya kuadhimisha miaka mitano ya huduma ya Mpawa yenye lengo la kuwahusisha kifedha wateja wake kwa kuwazawadia. Promosheni hiyo imefanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika droo hiyo mwakilishi wa benki ya CBA Maria Marbella, amesema kuwa watumiaji wa M-Pawa wamepanda kwa kasi kufikia milioni 8.5 tangu izinduliwe, huku wengi wa wateja hao wakiwa wafanya biashara wanawake, vijana na mamillioni ya watanzania, hasa maeneo ya vijijini ambapo huduma za benki ni za kiwango kidogo kwasababu ya ukosefu wa taasisi za benki au upungufu wa mahitaji ya kifedha.

Amesema mshindi wa kwanza wa promosheni hiyo atazawadiwa milioni 15 kwenye droo ya mwisho hivyo amesisitiza watumiaji wa Mpawa kuweka akiba na kurejesha mikopo mapema ili waweze kupata nafasi ya kushinda.

“Kampeni hii ya miaka mitano ya Mpawa imelenga kudumu kwa wiki sita na leo ikiwa ni droo ya tatu, tumekua na zaidi ya washindi 1,000 mpaka sasa tangu ilipoanza, ambapo baadhi ya washindi wameondoka na mara mbili ya akiba ya kuanzia na shilingi 1,000 mpaka shilingi 200,000 za Kitanzania, simu za kisasa, vocha pamoja na zawadi nyingine huku washindi wengine wakiongezeka kwenye droo zilizobaki.”amesema Marbella.

“Huduma hii ya Mpawa imeleta mapinduzi ya kibenki ambayo inaruhusu watumiaji wetu kuweka akiba kwa njia ya simu na kupata faida kutoka kwenye akiba yao na hatimaye kuongeza kiwango cha mikopo yao. Kutumia njia hii tunawawezesha wateja wetu kuendeleza mitaji yao kwa ajili ya baadae na kufikia baadhi ya ndoto zao.” amesema Marbella.

Aidha amefafanua namna ya kushiriki na kushinda katika droo hiyo ambapo amesema kuwa mteja wa M- Pawa anatakiwa kuweka akiba isiyopungua kiasi cha Tsh 1,000 za kitanzania, kukopa na kurudisha mapema mkopo wake na hapo papo atakuwa ameingia kwenye droo na kujiwekea nafasi ya kushinda.

Baadhi ya washindi wa droo hiyo namba 1, 2 na 3 ni Mangu Zanura, Nyerenga Rahim, Robert Tuisenge, Mwafumba Martha, Ayilla Agness, Kayombo Hilda, Mollel Charity, Gwandu Elizabeth, Agust Emannuel, Tezeyo Abinal, Mwita Joseph, Haule Reginberti, na Kabona Fadhili, pamoja na wengine wengi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles