27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli aamsha mzuka upya Stars

Elizabeth Hombo –Dar es salaam na Ramadhan Hassan-Dodoma

RAIS Dk. John Magufuli amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwenda nchini Misri, kwa ajili ya kuongeza hamasa katika kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars, inayoshiriki fainali za mataifa ya Afrika (AFCON).

Mkuu huyo wa nchi alitoa kauli hiyo jana Kigamboni  jijini Dar es Salaam, wakati akizindua mitambo ya gesi ya Kampuni ya Taifa Gas Ltd.

Agizo hilo la Rais Magufuli lilitokana na hatua ya Makonda kumwomba kiongozi huyo wa nchi atoe neno kuhusu timu hiyo baada ya kufungwa mabao 2-0 na Senegal katika mchezo wa kwanza wa fainali hizo uliochezwa Jumapili iliyopita.     

“Makonda umesema unataka kwenda Misri, nakutuma nenda hata leo na kawaambie wachezaji wasikate tamaa kushinda kwao ndiyo ushindi wa Tanzania.

“Na hata wakishindwa pia tunashindwa wote, kufungwa magoli mawili kusiwakatishe tamaa kwa sababu ni mwanzo sio mbaya.

“Kwanza wamefungwa tugoli tuwili tu na timu kubwa kama ile yenye wachezaji wengi Ulaya, nina imani watafanya vizuri tuendelee kuwaombea na kuwashingilia,”alisema Rais Magufuli.

Aidha, aliwatia moyo wachezaji wa Taifa Stars kwa kuwataka waendelee kupambana, licha ya kuanza vibaya.

“Mwanzo sio mbaya kwa kufungwa na timu inayoongoza Afrika tena kwa kufungwa 2-0 na Senegal ambayo wachezaji wao wote wakiwa wanacheza Ulaya,” alisema.

Alisema huu ni muda wa wachezaji wa kikosi hicho kupewa moyo ili waendelee kupambana na kufanya vizuri katika fainali hizo.

“Wachezaji wapewe moyo kwa sababu wakifungwa tunafungwa Tanzania na wakishinda basi inashinda Tanzania, kwenye uwanja wa mpira kuna kushinda na kushindwa sisi tutaendelea kuwaombea,”alisema Rais Magufuli.

Taifa Stars kwa sasa inajiandaa na mchezo wa pili dhidi ya Kenya utakaochezwa kesho.

Katika hatua nyingine,Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema baadhi ya viongozi wa serikali wamemdanganya hadharani Rais Magufuli, kuwa wabunge waliokwenda Misri kuishangilia Taifa Stars waliwadhihaki wachezaji.

Kauli hiyo ya Spika aliitoa jana jioni, baada ya Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zito Kabwe kuomba muongozo kwa kutumia kanuni ya 68 (7), kuhusu jambo lililotokea mapema bungeni.

Zitto alilazimika kuomba muongozo huo, baada ya Spika Ndugai kutoa ufafanuzi kwamba hakuna mbunge yeyote aliyewadhihaki wachezaji wa Taifa Stars baada ya mchezo wake na Senegal.

“Mheshimiwa Spika, kwa kutumia kanuni 68 (7), kuhusu jambo lililotokea bungeni mapema. Umeelezea jambo ambalo limetokea nje ya bunge kuwa mmoja ya viongozi wa serikali kuwabagaza wabunge waliokwenda Misri.


“Spika, umetoa maelezo kama sio muhimili wa serikali, naomba muongozo wako utoe kauli ili asije akatokea yeyote kuwabagaza wabunge.


“Kama kawaida yako umekuwa huruhusu muhimili wa bunge kutoruhusu kutomaswa, kudharauriwa, ni kipi kilichokupata utoe kauli kama ya kujitetea?. Toa kauli kama muhimili sio kama unajiteteta mbele ya kiongozi mdogo wa serikali.


Mara baada ya mbunge huyo kuomba muongozo huo, Spika Ndugai, alijibu kwa kuwaomba wabunge kutolikuza jambo hilo.
“Naomba tusilikuze jambo hili kabisa. Kama wabunge tungekuwa na mawazo kama wachezaji wana makosa, isingewezekana wabunge wengine 30 kwenda Misri. Ni bahati mbaya sana, kwamba tuna viongozi wa serikali, wanadiriki kumdanganya Rais hadharani.


Aliongeza: “Kiongozi wa serikali unapoongea mbele ya Rais, jipange, ongea ukweli mtupu mbele ya Mwenyenyezi Mungu. Na sisi hatutamani kusema, natamani kufunguka kidogo…inatosha..inatosha.

“Nasema wazi bahati mbaya kijana wetu huyu hajitambui, hajielewi kwa sababu ana nguvu aliyonayo ana makundi ya vijana kwenye mitandao ambao wanaweza kumtukana Spika, lakini tuache,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles