28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wema amaliza siku saba za kukaa gerezani

Na Kulwa Mzee, Dra-es-salaam

MSANII wa Filamu nchini, Wema Sepetu leo amemaliza siku saba za kukaa Gereza la Segerea baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuamuru aende mahabusu tangu Juni 17 mwaka huu.

Wema anaekabiliwa na mashtaka ya kuchapisha video ya ngono alibubujikwa na machozi mara baada ya amri hiyo kutolewa mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde.

Uamuzi wa kumpeleke Wema mahabusu ulifikiwa baada ya mshtakiwa huyo aliyekuwa anadaiwa kuruka dhamana kufikishwa mbele ya mahakama.

Akiiwakilisha Jamhuri Wakili wa Serikali, Glory Mwenda alidai mshtakiwa alikamatwa na kufikishwa mahakamani baada ya kuruka dhamana na mahakama kutoa hati ya kumkamata Juni 11 mwaka huu.

Hakimu Maira alisema mshtakiwa hakufika mahakamani Mei 14 mwaka huu bila taarifa na Juni 11 pia hakufika hivyo alimtaka kujieleza kwanini hakuhudhuria mahakamani na kwanini asifutiwe dhamana.

Akijieleza Wema alidai Mei 14 alisafiri kikazi kuelekea Morogoro akamjulisha Wakili wake, Ruben Simwanza na Juni 11 mwaka huu alifika mahakamani lakini aliumwa.

“Nilishindwa kupanda mahakamani, ninapofika kwenye siku zangu huwa napata maumivu makali, nilienda kuchoma sindano ya maumivu, nikapumzika kisha nikarudi nyumbani.

“Nilienda kuchoma sindano Hospitali ya Mbuyuni karibu na makaburi ya Kinondoni, nilifanyiwa upasuaji wa kizazi India hivyo maumivu yanatokea kila mwezi, naomba msamaha Mheshimiwa,”aliomba Wema.

Akijibu Wakili wa Serikali, Glory Mwenda alidai ni kweli mshtakiwa hakufika mahakamani kwa siku hizo lakini siku zote za kesi amekuwa akitoa taarifa hivyo aliiomba mahakama impe onyo kwa kutohudhuria sababu imeleta usumbufu.

Glory alidai siku nyingine asipofika wadhamini wake wafike kumwakilisha.
Wakili wake, Ruben aliomba Mahakama imsamehe mteja wake kwa usumbufu uliojitokeza na kuahidi kwamba hautajirudia.
“Tunaomba busara ya mahakama mshtakiwa abaki na dhamana yake,”alidai Ruben.

Hakimu Kasonde baada ya kusikiliza hoja za pande zote alisema atazizingatia pamoja na kiapo cha Wema kilichowasilishwa mahakamani hapo.

Alisema hawezi kutoa uamuzi siku hiyo kwani alikuwa na kazi nyingine, akaahidi kutoa uamuzi leo kisha aliamuru mshtakiwa akae mahabusu hadi leo atakapotoa uamuzi wa ama aendelee kuwa nje kwa dhamana ama amfutie dhamana.

Hati ya kumkamata Wema ilitolewa Juni 11 baada ya upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili Silvia Mitanto kudai kwamba mshtakiwa hayuko mahakamani na hakuna taarifa yoyote.

Wakili wa utetezi, Ruben Simwanza, alidai mshtakiwa alifika Mahakamani lakini kaumwa hivyo ameshindwa kuingia katika chumba cha Mahakama.

Mahakama ilitoa hati ya kumkamata mshtakiwa kwa sababu kama alifika alishindwa nini kuingia mahakamani.

Wema anakabiliwa na shtaka moja la kuchapisha video ya ngono katika mtandao wa kijamii. Anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, ambapo alisambaza video za ngono kupitia akaunti yake ya Instagram, picha ambazo inadaiwa kuwa haina maudhui.

Alidai Wema ambaye ni mkazi wa Mbezi Salasala, anamiliki mtandao wa kijamii wa Istagramu wenye jina la Wemasepetu.

Alidai siku hiyo ya tukio, mshtakiwa alirekodi video ya ngono ambayo haina maudhui kupitia simu yake ya kiganjani, akitumia laini ya Vodacom.
Baada ya kurekodi video hiyo, Oktoba 25, 2018, mshtakiwa aliisambaza katika akaunti yake ya Istagram, wakati akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Video hiyo aliyorekodi Wema, ilikuwa inaonyesha kuwa Wema alikuwa ananyonyana ndimi (denda) na mwanaume, huku akijua kuwa kitendo hicho ni kinyume na maadili ya Tanzania,”alidai.


- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles