KULWA MZEE-DAR ES SALAAM
Kesi ya kutakatisha fedha inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai na wenzake, yaibua utata mahakamani baada ya Jamhuri kuendelea kudai kwamba hawajapata fedha za kuita mashahidi.
Kesi hiyo imekuja leo Juni 18, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kusikilizwa ambapo Mahakama pamoja na washtakiwa walitaka iendelee lakini Jamhuri imekwama kwa kukosa mashahidi
Akiiwakilisha Jamhuri Wakili wa Serikali, Awamu Mbagwa, amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kwamba hawana mashahidi kwasababu mahakama haina fedha.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi Juni 20 na 25 kwa ajili ya kuendelea kusikiliza ushahidi ambapo Juni 3 Jamhuri kwa mara nyingine ilikwama kuita mashahidi kutoka nje ya Dar es Salaam kwa sababu mashahidi watano waliotoa ushahidi hawajalipwa stahiki zao.
Katika kesi ya msingi, Gugai na mwenzake, wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali.
Inadaiwa kuwa akiwa Takukuru Dar es Salaam, Gugai alikuwa akimiliki mali za zaidi ya Sh3.6 bilioni ambazo hazilingani na kipato chake huku akishindwa kuzitolea maelezo.
ya samaki yanasikitisha, ni kweli sheria zitafuatwa!