22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mahiga afafanua sheria ya mirathi

RAMADHAN HASSAN

Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Agustine Mahiga amesema kuwa hakuna sheria inayompa mgane haki zaidi ya mjane au kwa namna yoyote kuonesha ubaguzi na kwamba sheria zinaeleza namna mali inavyopaswa kugawiwa kwa wanufaika huku ikiainisha kila mnufaika na kiwango anachopata.

Ametoa kauli hiyo bungeni leo Juni 18, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Silafu Maufi (CCM) aliyetaka kujua ni kwa nini mjane asiandikwe jina lake kwenye hundi na asimame na watoto wake kwa kupewa haki ya kusimamia mirathi.

Akijibu, Dk Mahiga amesema utaratibu unaofanyika unamtaka msimamizi wa mirathi kuwasilisha mchanganuo wa malipo na hundi huandikwa kwa wanufaika wote pasipo kujali jinsia zao.

Amesema pamoja na kuwa na Sheria nzuri, kumekuwa na uelewa mdogo miongoni mwa baadhi ya wananchi kuhusu sheria, kanuni na taratibu zinazohusu utaratibu wa mirathi.

“Wizara yangu kupitia RITA na wadau mbalimbali imekuwa ikitoa elimu kwa makundi mbalimbali kuhusu mirathi na itaendelea kubuni mbinu zitakazosaidia ili elimu ya hiyo iwafikie wananchi wengi zaidi” amesema.

Ameongeza kuwa sheria za nchi zinatambua kuwa mirathi na usimamizi wake unaweza kuongozwa na sheria ya kiislamu au Sheria ya India ya mwaka 1885 kwa wasiokuwa waislamu na kwamba matumizi ya sheria hizo yanaangalia maisha ya marehemu, dini na namna marehemu alivyozikwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles