FLORENCE SANAWA, MTWARAÂ
Mahakama ya wilaya ya Nanyumbu mkoani mtwara imemtia hatiani mwenyekiti wa kitongoji cha elimu kijiji cha Chitowe, Shaibu Mussa akiwa na Afisa mtendaji wa Kata hiyo Walle Mlaponi, kwa kosa la kuomba rushwa ya shilingi 60,000.
Akitoa Hukumu hiyo leo Juni 17, hakimu mfawidhi Wilaya ya Nanyumbu Godfrey Anyimike amesema kuwa Mshtakiwa Shaibu Mussa amehukumiwa kwenda jela Miaka Mitatu au kulipa faini shilingi ya shilingi 500,000 kinyume cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa kifungu namba 15(1)(a) 11/2007 ambapo ameshindwa kulipa faini hivyo amepelekwa gereza la wilaya ya Masasi kutumika adhabu yake.
Inadaiwa kuwa mei 31, 2017 Mlaponi akiwa na Shaibu Mussa walimkamata na kumfungia Katika ofisi ya kijiji cha chitowe Hadija Manubi kwa kosa la kumtukana mwenyekiti wa kitongoji cha elimu walipokuwa Katika zoezi la kuchangia ujenzi wa zahanati ya kijiji ambapo walitumia nafasi hiyo kuomba rushwa.
Awali shtaka hilo lilifunguliwa na mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Cecilia Nshiku, Desemba 20 mwaka jana ambapo akiwa na afisa mtendaji wa kata ya nanyumbu Mlaponi alishtakiwa kwa makosa mawili ya kuomba na kupokea rushwa kinyume cha sheria ya Takukuru.
January 25 mwaka huu Mlaponi alisomewa mashtaka hayo na kukiri ambapo alihukumiwa kwenda jela Miaka mitatu au kulipa faini ya shilingi 1,000,000 kiasi ambacho alilipa chote.
Awali ilidaiwa kuwa mei 31, 2017 Walle Mlaponi akiwa afisa mtendaji kata ya nanyumbu akiwa na mwenyekiti wa kitongoji cha Elimu Shaibu Mussa walimkamata na kumfungia Katika ofisi ya kijiji cha chitowe Hadija Manubi kwa kosa la kumtukana mwenyekiti wa kitongoji cha elimu walipokuwa Katika zoezi la kuchangia ujenzi wa zahanati ya kijiji ambapo walitumia nafasi hiyo kuomba rushwa.