Safina Sarwatt, Kilimanjaro
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imesema ni lazima kwa wafanyabishara wakati na wadogo nchini kurasimisha biashara zao ili iwe rahisi kutambulika kitaifa na kimataifa.
Akizungumza na Mtanzania Digtal leo Juni 10, Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa BRELA, Bakari Mketo amesema Tanzania ina wajasiriamali wengi ambao bado hawajarasimisha biasahara zao.
Ameisema kuna faida nyingi sana kwa wajasiriamali kurasimisha biashara ambazo ni kuwasaidia kuwapa kitambulisho na leseni, wakati nchi huu ambao inaelekea katika uchumi wa viwanda lazima biashara zote nchini ziwe zimerasimishwa.
Amesema kuwa kurasimisha  biashara ni kuipa kitambulisho ambacho ni muhimu sana kwasababu ili mfanyabiashara aingie  katika ushindani wa tenda za kazi  lazima awe amesajiliwa BRELA na kama  biashara  au kampuni haijasajiliwa haitakuwa na sifa.
Naye Msajili Msaidizi wa Kitengo cha Ubunifu wa BRELA, Suzan Senso amesema changamoto kubwa ni uelewa mdogo wa wafanyabishara kutokana na kwamba kwa upande wa Vikoba na Saccos wakisajiliwa kwa maendeleo ya jamii basi wanajua wamemaliza.