Francis Godwin, Iringa
Wanafunzi wawili wa darasa la saba kutoka Shule ya Southern Highlands Mafinga mkoani Iringa ambao waliondoka nchini wiki mbili zilizopita kwenda nchini Finland kuwakilisha shule za Tanzania kwenye kongamano la mazingira la shule za msingi duniani wamerejea nchini na tamko kuhusu uhifadhi was mazingira.
Kiongozi wa wanafunzi hao Kitova Mungai ambae ni mkurugenzi wa shule hiyo amesema wanafunzi hao Mariam Wambura na Stephen Sanga wamewasili jana jioni na wanategemea kuliwasilisha tamko hilo la dunia juu ya mazingira ambalo wawakilishi wa nchi zote wamekabidhiwa.
“Tumerudi salama jana jioni kutoka Finland kwenye Word Summit Of Climate (WSSC 2019) tunashukuru wote waliofanikisha safari yetu hasa timu ya 4H clubs Tanzania na ENO na waandaaji wa kongamano,” amesema Kitova.
Amesema kongamano hilo la siku 10 la wanafunzi kuhusu utunzaji mazingira limehitimishwa na tamko la wanafunzi kuhusu utunzaji wa mazingira tamko ambalo litawezesha dunia kuwa katika hali nzuri ya ustawi wa mazingira duniani.
“Tamko hilo limelenga kuhamasisha shule na jamii kuendelea kutunza mazingira ili kuwezesha kizazi cha baadaye kuishi katika mazingira salama yasiyo na uharibifu wa mazingira,” amesema.
Pamoja na Mambo mengine, Mungai amesema Shule hiyo imekuwa ikijihusisha na utunzaji mazingira ambapo wamekuwa wakiwafundisha wanafunzu masomo ya ujasiriamali na utunzaji wa mazingira kwa kuotesha miche ya miti na kuisambaza maeneo mbali mbali ya shule.
“Kutokana na kazi hiyo ya utunzaji mazingira ndiyo iliyowezesha wanafunzi wetu kuteuliwa na waandaaji wa kongamano hilo kwenda nchini Finland kushiriki kongamano hilo la dunia kwa niaba ya shule zote Tanzania.