NEW YORK, MAREKANI
KIONGOZI wa serikali ya Ujerumani, Kansela Angela Merkel, ametunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima ya Chuo Kikuu maarufu cha Harvard. Rais wa Chuo cha Havard, Larry Bacow, aliyemtunukia Merkel tuzo hiyo amemueleza Kansela huyo wa Ujerumani kama mwanasiasa mwenye nguvu barani Ulaya.
Taarifa ya chuo hicho imemwelezea Merkel kwa matamshi yake kwa kusimama kidete wakati wa mgogoro wa wakimbizi ulioanza mwaka 2015 nchini Ujerumani, wakati aliporuhusu idadi kubwa ya wakimbizi na kukabiliwa na ukosoaji mkubwa nchini mwake.
Kwenye hotuba yake kwa wanafunzi, wakati wa mahafali ya 368 ya chuo hicho cha Havard, Merkel aliwaonya wanafunzi dhidi ya kuchanganyikiwa na kuchukulia uongo kuwa ukweli na ukweli kuwa ni uongo.