30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

CUF kupinga matokeo ya ubunge majimbo sita

NA PATRICIA KIMELEMETA, DAR ES SALAAM

CHAMA cha Wananchi (CUF) kinatarajia kufungua kesi katika mahakama mbalimbali nchini kupinga matokeo ya majimbo sita katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari  Dar es Salaam jana, Ofisa wa Haki za Binadamu na Sheria wa CUF, Mohamed Mluya, aliyataja majimbo hayo kuwa ni   Lindi Mjini, Newala, Mtwara Vijijini, Pangani, Mbagala na Tabora Mjini ambayo uchaguzi wake uligubikwa na dosari mbalimbali.

Alisema miongoni mwa dosari hizo ni   kutokuwapo  taarifa sahihi za idadi ya wapigakura, idadi ya vituo vya kupigia kura na kuongezeka kwa karatasi za kupigia kura jambo ambalo ni kinyume na taratibu ya sheria za uchaguzi.

“Tayari wanasheria wetu wamekaa na kuangalia dosari zilizojitokeza kwenye majimbo hayo   tuweze kuwasilisha mahakamani kwa ajili ya kupinga matokeo, lengo ni kuhakikisha haki inatendekea,” alisema Mluya.

Alisema  kutokana na hali hiyo, chama hicho kitawasilisha pingamizi hizo kwenye Mahakama Kuu za Kanda    kutetea ushindi wa majimbo hayo ambayo wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameibuka washindi.

Mluya alisema hadi sasa zaidi ya wanachama 43 wa chama hicho waliokuwa wakipinga matokeo hayo katika maeneo mbalimbali nchini wamekamatwa jambo linaloonyesha wazi   haki haijatendeka.

Ofisa huyo ameziomba mahakama kutenda haki wakati wa kusikiliza kesi hizo ziweze kutoa ushindi kwa wagombea wa chama hicho ambao wanakubalika na wananchi.

Aliyekuwa mgombea ubunge wa chama hicho Jimbo la Tabora, Peter Mkufya, alisema kumejitokeza dosari mbalimbali ikiwamo ya kutokuwapo   idadi kamili ya vituo vya kupigia kura jambo ambalo limeleta shaka.

“Idadi ya wapigakura waliojiandikisha ni 380,000 lakini wakati wanatangaza matokeo msimamizi wa uchaguzi alisema wapiga kura walikuwa 400,000 wakati si kweli,” alisema.

Alisema baada ya kutangazwa mshindi wa CCM, mgombea huyo alimuomba msimamizi wa uchaguzi kurudia kuhesabu upya matokeo ya uchaguzi lakini alikataa.

“Baada ya kujitokeza kwa dosari nyingi tulimuomba msimamizi wa uchaguzi kurudia kuhesabu kura lakini walitukatalia na kutunyima kujaza fomu namba 16,” alisema Mkufya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles