29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Aubameyang awahofia Chelsea fainali Europa

LONDON, ENGLAND

Aubameyang awahofia Chelsea fainali Europa LONDON, ENGLAND MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang, amesema angependa  timu yake ingevaana na Frankfurt ya Ujerumani kwenye mchezo wa fainali ya Ligi ya Europa lakini si Chelsea.

Timu hizo mbili zinatarajia kuvaana kwenye mchezo wa fainali kama zitafanya vizuri kwenye michezo yao ya mwisho baada ya Arsenal kushinda nyumbani mabao 3-1 dhidi ya Valencia na Chelsea kulazimishwa sare ya bao 1-1 ikiwa ugenini dhidi ya  Frankfurt.

Katika Ligi Kuu England, Arsenal ilipoteza  ugenini dhidi ya Chelsea mchezo wa mzunguko wa pili kwa kufungwa mabao 3-2 Agosti mwaka jana baada ya washika bunduki hao kushinda mabao 2-1 Januari mwaka jana.

Aubameyang alisema asingependa kuvaana na vijana wa Maurizio Sarri kwa mara ya tatu na anahisi mchezo dhidi ya Frankfurt utakuwa wenye mvuto na changamoto nyingi.

“Tunafahamu Chelsea ni timu kubwa, lakini tunakwenda kucheza fainali na tungependa kuvaana na Frankfurt kwa sababu tayari tulishacheza dhidi ya Chelsea.

“Nafahamu Frankfurt ni timu nzuri na kama ikifanikiwa kuvuka hatua ya fainali na tukakutana utakuwa mchezo mzuri na mgumu kila upande.”

Aubameyang kwa sasa amebakisha mabao mawili kumfikia kinara, Mohamed Salah wa Liverpool, katika mbio ya kuwania tuzo ya kiatu cha dhahabu msimu huu baada ya kufikisha mabao 19 ya Ligi Kuu England.

“Tupo kwenye mapambo makali. Kuna washambuliaji wenye uwezo Ligi Kuu England. Matumaini yangu hawataweza kuendelea kufunga, lakini nina uwezo wa kuendelea kufanya hivyo. Kama sitaweza kufunga haitakuwa tatizo.

“Lakini bado tuna michezo miwili ya Ligi Kuu hivyo nina nafasi ya kufunga. Nilishinda kiatu cha dhahabu mara mbili nikiwa Ujerumani. Mimi pamoja na Robert Lewandowski, tuliwahi kufungana idadi ya mabao 30, lakini hatua ya mwisho niliweza kuongeza bao baada ya kufunga kwa mkwaju wa penalti.

“Ukiwa mshambuliaji inakuwa na maana kubwa na kama ukitaka kuwa bora lazima ushinde kiatu cha dhahabu,” alisema Aubameyang.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles