32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wanaharakati waandamana kulaani ukatili wa Saudia

LONDON, UINGEREZA

WANAHARAKATI na watetezi wa haki za binadamu wamefanya maandamano nje ya Ubalozi wa Saudi Arabia katika mji mkuu wa Uingereza, London, kulaani ukatili wa hivi karibuni wa watawala wa Saudi Arabia, baada ya kuwanyonga watu 37 ambao ni Waislamu wa madhehebu ya Shia.

Mamia ya wanaharakati hao, wakiwamo wapinzani na wakosoaji wa utawala wa Saudia walifanya maandamano hayo jana nje ya ubalozi wa Saudia mjini London, wakitaka serikali ya Uingereza na nchi nyingine za Ulaya zivunje kimya chao kutokana na makosa ya jinai yanayofanywa na Saudi Arabia dhidi ya haki za binadamu. 

Waandamanaji hao wamesema ukatili wa Saudia umevuka mipaka na kukanyaga sheria zote za kimataifa, na kwamba kitendo hicho cha kuwanyonga raia 37, wakiwamo watoto wadogo, mlemavu na wanazuoni, na kisha kuusulubisha mwili wa mmoja wa Waislamu hao hadharani hakikubaliki.

Duru za kisheria na haki za binadamu zinasema kuwa hii ni mara ya pili ndani ya wiki moja kwa watetezi hao wa haki za binadamu na wakosoaji wa utawala wa Saudi Arabia kuandamana mjini London.

Mashirika na taasisi za kimataifa pamoja na wanaharakati wa masuala ya kijamii wanaendelea kulaani jinai ya hivi karibuni ya utawala wa Aal Saud wa Saudi Arabia ya kuwaua kwa umati raia 37 wa nchi hiyo.

Harakati za Mapambano ya Kiislamu za Hizbullah ya Lebanon na Hamas ya Palestina, shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty International na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ni miongoni mwa asasi za kimataifa zilizolaani hatua hiyo ya watawala wa Saudia kutumia kisingizio cha kupambana na ugaidi kuwanyonga kwa umati Waislamu wa Kishia, zikisisitiza kuwa utawala huo wa kifalme hauheshimu thamani ya utu. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles