32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Zahera atamba kuinyoa Alliance kwa kikosi kilichomenyana na Lipuli

Lulu Ringo, Dar es Salaam

Kocha Mkuu wa Timu ya Yanga, Mwinyi Zahera, amesema atatumia mfumo ule ule uliotumika katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Timu ya Lipuli (Wanapaluhengo) ili kuimaliza Alliance FC, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam, (ASFA) utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Machi 29, Zahera amesema licha ya kupoteza mchezo na Lipuli katika mchezo wao wa Ligi Kuu, kikosi chake kilikuwa sawa sawa na kilicheza mchezo mzuri ila wachezaji walikosa ujasiri wa kutumia nafasi nyingi walizozipata na kuruhusu Lipuli kuwafunga kwa nafasi pekee waliyoipata mbele ya lango la Yanga.

“Katika mechi ile, timu ilicheza vizuri tulipata nafasi zaidi ya mara tano, lakini hatukupata bahati ya kufunga na wenzetu walipiga shuti moja tu lililowapatia ushindi wa goli 1-0.


“Shida ya wachezaji wangu hawakujiamini kwa nafasi walizokuwa wakipata, tumefanya uchambuzi kwa pamoja wa ule mchezo, nimewaambia wachezaji wangu wakicheza kama walivyocheza na Lipuli katika mchezo wa kesho basi tutashinda bila wasiwasi ila tuna kazi kubwa zaidi maana mchezo wa Ligi Kuu wa mwisho na Alliance hatukufanya vizuri sana,” amesema Zahera.

Timu ya Alliance na Yanga zitatoshana nguvu kesho ikiwa ni mchezo wao wa tatu tangu Alliance ipande daraja kucheza Ligi Kuu Bara.

Mchezo wa kwanza ulichezwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaa ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa goli 3-0 na mchezo wa pili ulichezwa katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza na Yanga kutoka kifua mbele kwa goli pekee lililofungwa na Amis Tambwe dakika ya 74.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles