Na Mwandishi Wetu
Maelfu ya waalimu wa Morocco wameandamana katika mji mkuu, Rabat, wakidai kuboreshewa mikataba yao.
Pamoja na hilo la kudai kupatiwa mikataba ya kudumu, walimu hao pia wanataka wawekewe mazingira mazuri ya kufanyia kazi pamoja na kupinga gharama za maisha zinazoongezeka.
Waandamanaji hao wamekataa mapendekezo ya Serikali ili kukomesha mgogoro huo.
Lakini pia waalimu wa mikataba ya muda mfupi, ambao ni zaidi ya miaka ya 20 na 30, wamekuwa wakipifanya migomo mara kwa mara siku za hivi karibuni zikidai kubadiishwa kwa hali ya mikataba iliyo sasa.