BAMAKO, MALI
WATU 134 wameuawa baada ya kijiji kimoja kilichoko katikati ya Mali kushambuliwa, kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.
Kupitia taarifa aliyoitoa usiku wa kuamkia jana, Guterres ameeleza kuwa watu waliokuwa na bunduki walikishambulia kijiji cha Ogossagou Peulh katika eneo la Mopti katikati ya Mali.
Watu 55 pia walijeruhiwa na washambuliaji, ambao bado hawajatambuliwa.
Guterres ameeleza kushtushwa na kusikitishwa na shambulizi hilo la juzi asubuhi dhidi ya wanakijiji wakiwemo wanawake na watoto.
Nchi hiyo ya Afrika Magharibi imekumbwa na mashambulizi kutoka kwa makundi yenye silaha tangu mapinduzi ya mwaka 2012