27.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

IDADI YA WALIOPOTEZA MAISHA KWA KIMBUNGA IDAI YAZIDI KUONGEZEKA MSUMBIJI

Na Mwandishi Wetu

Idadi ya waliopoteza maisha kutokana na kimbunga Idai kilichoikumba eneo la kusini mwa Afrika zaidi ya juma moja lililopita,imeongezeka kwa kasi siku ya Jumamosi.

Idadi ya waliothibitishwa kupoteza maisha nchini Msumbiji imeongezeka kutoka 242 mpaka 417, Waziri wa Ardhi na Mazingira nchini humo Celso Correia ameeleza.

Idadi hii mpya inafanya waliopoteza maisha Msumbiji, Zimbabwe na Malawi kufikia 700 lakini pia idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka zaidi.

Kimbunga kimeua takribani watu 259 nchini Zimbabwe na Malawi 56. Watu walipoteza maisha kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha mafuriko.

Lakini Umoja wa Mataifa limesema maafisa wataweza kutathimini madhara pale maji yatakapopungua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,903FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles