25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kitu gani kilisababisha muwe pamoja katika uhusiano?

ZIPO na lawama nyingi zinazotolewa na baadhi ya watu kutokana na mienendo ya wapenzi wao. Wapo wanaona hawatendwi haki, wengine wanaona kama wanajipendekeza kwa wapenzi wao na nyinginezo nyingi.

  Ila majibu ya maswali haya yanaweza kupatikana pia kama kila mmoja atajiuliza kuwa amempata vipi mpenzi wake. Ni vitu gani vilivyo sababisha wao wawe katika uhusiano waliopo.

  Hapana. Hapa sizungumzii mazingira kama vile, kukutania sokoni, baa, kwenye nyumba za ibada au hata disko. Ninachozungumzia ni kitu gani kilisababisha uwe naye katika uhusiano.

   Uhusiano mengi yanaanzishwa kutokana na sababu dhaifu zisizo za kimapenzi hali inayochangia kutokuwa na uwezo wa kuhimili kukaa muda mrefu. Ikiwa mpenzi wako ulimpata kwa sababu eti alikuonea huruma baada ya kumuhangaikia kwa kipindi kirefu, jua upo katika janga.

   Kama huyo unayemuita sweetie alikukubali eti kisa unatoka familia flani fahamu umeumia. Mapenzi hayako hivyo.

   Siri ya kudumu katika uhusiano ni kila mmoja kuwa na hisia na mwenzake. Hauwezi kuwa na amani katika uhusiano yako kama mwenzako aliamua kuwa na wewe eti kwa sababu ukivaa unapendeza sana.

 Mapenzi siyo ‘fashion show’. Waliongia katika mapenzi kwa sababu hiyo leo tunawaona. Leo ndiyo hao mbali na kupendeza kwao wanaonekana kama vinyago tu, mbali na magari yao wanaonekana kama wendawazimu mbele ya wenzao.

   Mapenzi si suala la kuangalia sana vitu vya nje. Anayefanya hivyo jua kinachomsukuma siyo mapenzi. Ni tamaa! Wewe mpenzi wako umempata vipi?

 Hata kama umempata disko au chuoni ni kitu gani kimemsukuma kuwa na wewe? Jiulize tu. Ila kama alihitaji kuwa na wewe eti kwa kuwa ulikuwa unacheza vizuri au ulikuwa unaongoza darasani jua umeumia.

Hapo siyo mapenzi. Kivipi ahitaji kuwa na wewe eti kwa kuwa kila siku unakuwa namba moja, je hiyo namba akishika mwingine maana yake si utaachwa hapo au? Zote hizo tamaa.

   Tamaa za kujinadi natoka na mburula ambaye ndiyo kichwa wetu. Bila kuangalia mmekutania wapi, misingi ya mapenzi ni lazima iangaliwe ili kila mmoja aweze kuwa katika uhusiano wa kweli na siyo mfano wa mapenzi.

Hisia za dhati baina ya wahusika ndiyo zinafaa kuwa kigezo cha kwanza cha wao kuungana. Siyo sijui natoka masaki, mara nafanya kazi ‘airport’ hapana. Hisia ndiyo msingi wa kweli wa uhusiano baina yenu.

    Uhusiano wa kweli hayapatikani kwa kuoneana huruma wala kwa kuwa wote mnaishi Osterbay. hapana. Nguvu ya uhusiano inaweza kuwaunganisha wale wa Masaki na Tandale kisha kusionekane tofauti baina yao.

 Katika mapenzi msomi na ngumbaru wote wanaweza kukaa meza moja na kuendelea kuheshimina. Suala ni hisia tu. Kama kweli wanahisia za kweli katika uhusiano hakuna kitakachofanya wajihisi tofauti.

   Kuwa  makini sana na huyo mpenzi wako uliyempata kisa ulimpa kazi kwa sababu anachofanya kwako ni kulipa fadhila na si kuwa anafurahia kuwa na wewe.

 Wewe kwake ni daraja tu katika kutimiza lengo lake katika maisha ya kiutafutaji. Kuwa makini sana kabla hujaanzisha mahusiano.

   Tamaa zako za muda mfupi zisikufanye umkubali kisa anaomba kuwa na wewe, bila kujua kuwa anataka kuwa na wewe kisa wewe ni afisa wa mikopo na yeye ni mwenye uhitaji wa mkopo huo.

Ukiwa wake tu inabidi ukubali siku moja kuumia. Leo anaweza kuwa na furaha sana wakati anaanzisha uhusiano na wewe kwa sababu unaenda kumfanikishia mpango wake, ila jua ipo siku tu atakuona takataka.

 Ndivyo ilivyo. Mapenzi si rahisi sana kwa mtindo huo. Hapo unaweza kuambulia ngono na sifa nyngi ila hisia zisiwe kwako. Umempata vipi mpenzi wako?

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles