Mwandishi Wetu
Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Uhusiano wa Nchi za Kusini (UNOSSC), Umoja wa nchi Afrika, Karibian na Pasifiki (ACP) na nchi mbalimbali zimeipongeza Tanzania kwa kufanikiwa kulinda rasilimali zake ikiwamo kudhibiti utoroshaji fedha haramu nje ya nchi.
Akiwasilisha mada kuhusu juhudi za Tanzania katika mkutano wa South-South nchini Argentina, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro, amesema mafanikio hayo ni matokeo ya utashi wa kisiasa ambayo Tanzania inao.
“Jumuiya za kimataifa na nchi mbalimbali zimemsifu na kumpongeza Rais John Magufuli, kwa kuongoza mabadiliko ya kiuchumi Tanzania ambayo yameleta mafanikio katika utekelezaji wa Malengo ya Endelevu ya 2030 kama vile elimu bure, kuimarisha huduma za afya, ujenzi wa miundombinu na mkakati wa kuendeleza viwanda,” amesema Dk. Ndumbaro.