20.8 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Miaka 30 jela kwa kumbaka, kumpa mimba mwanafunzi

Derrick Milton, Simiyu

Mahakama ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, imemhukumu mtu mmoja kifungo cha miaka 30 kwa kumbaka na kumpa  mimba mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Maswa.

Mtuhumiwa huyo Sunzu Mpangala (27) mkazi wa kijiji cha Igunya kata ya Shishiyu wilayani Maswa amehukumiwa kifungo hicho leo Ijumaa Machi 22, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Maswa, Tumaini Marwa.

Mwendesha Mashtaka wa Jeshi la Polisi Inspekta Nassib Swedi, aliiambia mahakama mtuhumiwa alitenda kosa hilo Juni 12, mwaka janao katika kijiji cha Igunya kata ya Shishiyu.

Ilidaiwa mahamakani hapo kuwa  mshtakiwa huyo alikuwa akimfundisha mwanafunzi huyo wakati wa likizo akiwa anasubiria ajira kutoka serikalini kwani yeye alikuwa mhitimu wa Shahada katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Mshtakiwa huyo alipopewa nafasi ya kujitetea mahakamani hapo alikiri kutenda kosa hilo na kuiomba mahakama ijaribu angalau kumpunguzia adhabu kwa kuwa yeye hana wazazi na anategemewa na familia hoja ambayo haikufua dafu mbele ya mwendesha mashtaka ambaye aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mtuhumiwa huyo ili iwe fundisho kwake na watu wengine wenye tabia kama hizo za kukatisha ndoto za wanafunzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles