30.4 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

China kuupigia kura muswada wa sheria kuhusu uwekezaji wa kiigeni

BEIJING, CHINA

BUNGE la China wiki ijayo litaupigia kura muswada uliowekewa matumaini makubwa kuwa utaleta mabadiliko ya kimsingi kwa wawekezaji wa kigeni nchini hapa.

Hatua hiyo inatajwa huenda ikasaidia kulegeza mivutano ya kibiashara iliyopo na Marekani.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Bunge hilo, Zhang Yesui. muswada wa sheria ya uwezekezaji wa kigeni utafuatiliwa kwa karibu katika kikao cha kila mwaka cha wiki mbili cha Bunge la Taifa la China kitakachofunguliwa leo,.

Sheria hiyo ya uwekezaji inalenga kuyashughulikia malalamiko ya muda mrefu ya kampuni za kigeni.

Hata hivyo, nchi za Ulaya zimezungumzia shaka yao kuwa sheria hiyo inaelekezwa kuyafikia mapendekezo ya Marekani pekee kuhusu biashara.

Sheria hiyo itaondoa kigezo cha kampuni ya kigeni kutakiwa kuhamishia nyenzo zao za teknolojia kwa washirika wake wa China.

Kigezo hicho ni suala kuu katika mazungumzo ya kibiashara kati ya China na Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles