25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Pluijm: Yanga ‘speed 120’, haipungui

1687602_heroaNA JUDITH PETER, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans Van Der Pluijm, ameendelea kuwapa programu ya mazoezi wachezaji waliobaki kwenye kikosi hicho, huku akisisitiza spidi 120 waliyoanza nayo Ligi Kuu Bara haiwezi kupungua watakapoivaa Azam FC Oktoba 17, mwaka huu.

Wachezaji 10 wa Yanga wameitwa kuzichezea timu zao za Taifa, ambapo wamejiunga na kikosi cha Taifa Stars ambacho kitapambana na Malawi keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwaka 2018, nchini Russia.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu, wataendelea kuwakosa nyota hao hadi Stars itakapocheza mechi ya marudiano na Malawi Jumapili hii ugenini.

Nyota hao ni kipa Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela, Deus Kaseke, Simon Msuva, Haruna Niyonzima na Amissi Tambwe.

Kocha huyo raia wa Uholanzi aliliambia gazeti hili jana kuwa, hana wasiwasi wa kuwakosa nyota wake walioitwa kuzitumikia timu za taifa akiamini wanatambua majukumu yao ya uwanjani pamoja na kusoma mbinu ambazo zitasaidia kuipa klabu hiyo mafanikio makubwa.

“Tumejipanga kwa kila mechi Ligi Kuu hivyo tutaingia uwanjani tukiwa na asilimia kubwa ya ushindi, tangu tumeanza ligi Yanga imekuwa timu bora ndiyo maana tunataka kuendelea kudhihirisha hilo,” alisema.

Yanga jana jioni walifanya mazoezi kwenye uwanja wao wa Kaunda, lakini leo asubuhi wataendelea kujifua kwenye Uwanja wa Polisi Kurasini kusaka makali ya kuikabili Azam.

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika mchezo wa Ngao ya Jamii ambapo Yanga waliifunga Azam kwa jumla ya penalti 8-7 baada ya dakika 90 kumalizika bila kufungana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles