WASHINGTON, MAREKANI
BARAZA la Wawakilishi la Marekani linaloongozwa na Chama cha Democrat limepiga kura 248 dhidi ya 177 kuunga mkono azimio la kuacha kuiunga mkono Saudi Arabia katika mashambulio ya jeshi inayoyaongoza nchini Yemen.
Wabunge wamesema wana wasiwasi jinsi Marekani ilivyochangia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Yemen, ambavyo vimeua maelfu ya watu.
Wawakilishi waliopiga kura dhidi ya muswada huo wamesema kusimamisha msaada kwa Saudi Arabia kutaharibu uhusiano wa Marekani na washirika wa kanda Mashariki ya Kati.
Wwameonya itadhoofisha juhudi zake za kukomesha usambaaji wa misimamo mikali ya dini.
Ikulu ya Marekani imekuwa ikijitetea kuwa haina askari hata mmoja anayehusika moja kwa moja katika vita vya Yemen.